1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CANCUN:Kimbunga Dean chaikumba pwani ya Mexico na kuzusha hofu

21 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBX8

Kimbunga Dean kimeipinga pwani ya Mexico hii leo na kusababisha mvua kubwa katika eneo hilo la mwambao wa pwani ya Caribbean.

Kimbunga hicho kilifikia kiwango cha tano kwa vipimo vya kitaalam hapo jana huku kikiwa na upepo unakwenda kwa kasi ya kilomita 260 kwa saa.

Kulingana na Kituo cha kitaifa cha utabiri wa hali ya hewa cha mjini Miami nchini Marekani vimbunga 28 pekee ndivyo vimefikia viwango hivyo mpaka sasa kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa tangu mwaka 1886.

Athari za kimbunga hicho zilianza kuonekana kwenye rasi ya Yucatan na kusababisha vifo vya watu 9 kote kwenye eneo la Caribbean.

Hata hivyo kimbunga hicho kinatarajiwa kulipiga zaidi eneo la kusini lisilo na wakazi wengi linalopakana na nchi ya Belize.Eneo hilo liko kilomita 300 mbali ya hoteli ya kitalii ya Cancun

Kampuni ya mafuta ya serikali cha PEMEX imefunga viwanda vyake vyote kwenye eneo la Ghuba ya Mexico na kuwaondoa wafanyakazi wake wote.