1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Caracass: Rais wa Vernezuela, Hugo Chavez, anataka kutaifisha makampuni ya nishati na ya mawasiliano ya simu ya nchi yake.

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CBHk

Rais Hugo Chavez wa Venezuela anapanga kuliomba bunge la nchi yake limpe madaraka maalum ambayo yatamruhusu kupitisha sheria kwa amri yake. Katika hotuba yake ya televisheni alielezea mipango yake ya kujenga dola ya kijamaa na kuyataifisha makampuni ya nishati na mawasiliano ya simu. Rais Chavez ambaye alichaguliwa tena kuwa rais mwezi uliopita, alisema pia anapanga kuibadilisha katiba ya nchi ili kumaliza uhuru wa benki kuu ya nchi hiyo. Bwana Chavez ataapishwa kesho kuwa rais wa Venezuela kwa kipindi cha tatu.