1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyama vya CDU/CSU vyazindua kampeni

Sudi Mnette
3 Julai 2017

Kampeni za uchaguzi zimepamba moto nchini Ujerumani. Baada ya chama cha Social Democrat-SPD, hii leo vyama ndugu vya CDU/CSU vimebainisha mshikamano wao kwa kutangaza ilani yao kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Septemba.

https://p.dw.com/p/2fr0P
CDU und CSU stellen Wahlprogramm zur Bundestagswahl vor
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wa CDU pamoja na kiongozi wa CSU, Waziri Mkuu wa Jimbo la Bayern Horst SeehoferPicha: picture alliance/dpa/K. Nietfeld

Mwenyekiti wa chama cha Christian Democratic Union CDU kansela Angela Merkel na mwenzake wa chama kidogo cha Christian Social Union CSU, Horst Seehofer wameitangaza kwa pamoja ilani hiyo katika makao makuu ya chama  cha CDU, katika jengo la Kondrad Adenauer mjini Berlin, iliyopewa jina " "Kwa ajili ya Ujerumani  tunakopendelea kuishi na kwa nafasi."

CDU und CSU stellen Wahlprogramm vor Angela Merkel und Horst Seehofer
Viongozi wa vyama ndugu CDU/CSU vya UjerumaniPicha: picture alliance/dpa/M. Kappeler

Lengo la ilani hiyo ni kuwahakikisha wajerumani watakuwa na maisha bora zaidi, mhula mpya utakapomalizika, amesema kansela Angela Merkel anaeendelea kusema. "Ilani yetu kwa mustakbali wa Ujerumani inamaanisha neema na usalama kwa wote. Na tunataka maisha ya watu yawe bora zaidi kuliko naamna yalivyo hivi sasa, mhula unaokuja utakapomalizika.Tunaweza hadi mwaka 2025 kupunguza tena kwa nusu idadi ya wasiokuwa na kazi kkutoka asili mia 5.5 hivi sasa na kufikia asili mia chini ya 3...ikimaanisha kila mtu atakuwa na kazi."

Mbali na ajira ilani ya vyama ndugu vya CDU/CSU inazungumzia  pia jinsi ya kupunguziwa mzigo familia, mfumo wa digitali na sera ya maendeleo.

Baada ya mivutano ya miezi kadhaa kuhussu sera za kansela Merkel kuelekea wakimbizi na lawama na hujuma za papo kwa papo za Seehofer dhidi ya kansela Merkel, waziri mkuu wa jimbo la kusini la Bavaria, mwenyekiti wa chama kidogo cha CSU Horst Seehofer amesifu ushirikiano wa vyama vyao viwili katika kuratibu ilani hiyo."Kulikuwa na moyo wa ushirikiano wa dhati" amesema walipokuwa wanatangaza ilani hiyo. Amesisitiza anamuani kikamilifu kansela Merkel. Hata hivyo tofauti za maoni zingalipo bado kuhusiana na suala la wakimbizi. Kansela Merkel amesema wazi wazi kwamba hakubaliani na kiwango cha juu kichowekwa na Seehofer kuhusu idadi ya wakimbizi wanaoruhusiwa kuingia Ujerumani kwa mwaka. CSU wanapanga kutangaza msimamo wao kuhusiana na suala la wakimbizi katika ilani ya Bavaria itakayoshadidia msimamo wa chama hicho kinachowakilishwa katika maeneo ya kusini tu mwa Ujerumani. Hata hivyo hakufika umbali wa kushurutisha idadi ya wakimbizi na kujiunga CSU katika sereikali kuu ya muungano mjini Berlin. Seehofer anataka wakimbizi laki mbili tu  waruhusiwe kuingia Ujerumani kwa mwaka.

Katika sera ya koodi ya mapato vyama ndugu vya CDU/CSU wanataka kuwapunguzia raia mzigo wa Euro bilioni 15 kutoka kodi ya mapato. Malipo ya kugharaimia ujenzi mpya katika sehemu ya mashariki mwa Ujerumani au kodi ya mshikamano kama inavyojulikana, itafuatwa hatua baada ya hatua kuanzia mwaka 2020.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/KNA/AFP
Mhariri  Mohammed Abdul-Rahman