1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CDU na SPD vyapoteza umaarufu licha ya kushinda uchaguzi

Sylvia Mwehozi
2 Septemba 2019

Matokeo ya chaguzi mbili zilizofanyika Jumapili katika majimbo ya Ujerumani ya Saxony na Brandenburg, yanaonyesha kuwa vyama vya SPD na CDU vimepata ushindi na hivyo kusalia kileleni, licha ya umaarufu wake kupungua.

https://p.dw.com/p/3OrjR
Lantagswahlen Brandenburg Andreas Kalbitz AFD Jubel
Picha: Reuters/A. Schmidt

Chama cha Kansela Angela Merkel cha Christian Democrats CDU kimesalia kuwa chama chenye nguvu kwenye jimbo la Saxony kwa kuibuka na asilimia 32 ya kura. SPD imeendelea kuwa juu katika jimbo la Brandenburg kwa kujinyakulia asilimia 26.2 ya kura, ingawa imeporomoka toka asilimia 31.9 ya uchaguzi uliopita. Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, chama mbadala kwa Ujerumani AfD kimeibuka nafasi ya pili katika majimbo yote mawili na hivyo kujiimarisha zaidi. Chama hicho cha AfD kimetumia hasira ya wapiga kura kuhusiana na sera ya wahamiaji kuweza kujiimarisha zaidi katika eneo hilo la Ujerumani Mashariki ya zamani.