1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha CUF visiwani Zanzibar chamtambua Rais Karume

9 Novemba 2009

Huko Zanzibar, siasa zilitokota mwishoni mwa wiki, ambapo kulikuweko mkutano wa hadhara Unguja mjini.

https://p.dw.com/p/KS5O

Katika mkutano huo katibu mkuu wa Chama kikuu cha upinzani cha CUF, Seif Shariff Hamad, alitangaza kwamba chama chake sasa kinamtambua Amani Karume kuwa ni rais wa Zanzibar. Baada ya kutoa tangazo hilo kulitokea purukushani, ambapo wanachama wa CUF waliokuweko uwanjani walimpinga na kusema wao hawakubaliani na uamuzi huo. Mchana wa leo Othman Miraji alizungumza na Maalim Seif Shariff Hamad, na kwanza alifafanua juu ya tangazo lake na purukushani iliotokea: