1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha SPD na uteuzi wa mgombea ukansela

24 Machi 2008

Nchini Ujerumani,baadhi kubwa ya wafuasi wa chama cha SPD hawataki kumuachia kiongozi wa chama hicho Kurt Beck uamuzi wa kumteua mgombea ukansela atakaepambana na Kansela Angela Merkel katika uchaguzi ujao.

https://p.dw.com/p/DTeu
ARCHIV - Der SPD-Parteivorsitzende Kurt Beck (l) und Bundesaußenminister Frank-Walter Steinmeier unterhalten sich am Donnerstag (25.10.2007) im Congress-Centrum Hamburg (CCH) bei einer Veranstaltung der Friedrich-Ebert-Stiftung (Archivfoto vom 25.10.2007). Beck hatte vor knapp drei Wochen die Möglichkeit einer Links-Kooperation in Hessen angedeutet. SPD-Bundesvorstand und -parteirat hatten dann den Landesverbänden freie Hand gegeben. Danach hatte die hessische SPD-Landesvorsitzende Ypsilanti ihr Vorhaben öffentlich gemacht. Im SPD-Debakel um eine Regierungsbildung in Hessen bahnt sich möglicherweise eine überraschende Wende an: Die SPD-Landtagsabgeordnete Metzger erwägt, ihr Mandat niederzulegen. Zunächst hatte sie den Plan von Andrea Ypsilanti für eine von der Linken tolerierte rot-grüne Minderheitsregierung mit ihrem Veto verhindert. Foto: Maurizio Gambarini +++(c) dpa - Bildfunk
Mwenyekiti wa chama cha SPD,Kurt Beck(kushoto) pamoja na Waziri wa Nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier.Picha: picture-alliance/ dpa

Kwa mujibu wa matokeo ya kura ya maoni yaliyotangazwa siku ya Jumapili ,kiasi ya asilimia 91 ya wanachama wa SPD wanataka kupiga kura wenyewe kumchagua kiongozi atakaekuja kugombea wadhifa wa ukansela hapo mwakani.

Wakati huo huo makamu wa mwenyekiti wa chama hicho,Frank-Walter Steinmeier ambae pia ni Waziri wa Masuala ya Nje wa Ujerumani anasema,kabla ya kuanzisha midahalo ya kumteua mgombea wao,chama kinapaswa kueleza waziwazi mkondo wa kisiasa unaofuatwa na chama hicho.Amesema,chama hakina budi isipokuwa kudhihirisha kuwa ni chama kinachofuata sera za kati.Steinmeier anapinga kabisa kushirikiana na chama cha mrengo wa shoto Die Linke.Amesema kuwa baada ya uchaguzi mkuu utakaofanywa mwaka 2009,chama cha SPD hakitojaribu cho chote pamoja na Die Linke. Akasisitiza kuwa huo ni msimamo wa SPD na vivle vile ni msimamo wake binafsi.

Wakati huo huo kiongozi wa SPD,Kurt Beck amesema, atakapompendekeza mgombea ukansela,atazingatia mafanikio ya chama hicho.Akaongezea kuwa kiongozi atakaetoa changamoto kwa Kansela Angela Merkel katika uchaguzi wa mwaka 2009,atahitaji kuwa na uzoefu wa kisiasa na uwezo wa kuongoza.Beck akaeleza kuwa uamuzi wake utatangazwa baadae mwaka huu au mapema mwakani.

Lakini kura ya maoni imedhihirisha kuwa kutoka jumla ya raia 1,000 waliohojiwa,asilimia 87 wamepinga kumuachilia Beck kumteua mgombea ukansela.Yeye ameungwa mkono na asilimia 5 tu.Kiongozi huyo wa SPD alipoteza sana umaarufu wake,baada ya kuashiria uwezekano wa kufanywa majadiliano pamoja na chama cha Die Linke kinachoelemea mrengo wa shoto,katika jeribio la kutaka kuunda serikali ya jimbo la Hesse.Lakini hivi karibuni alisema ,vyama vya SPD na Die Linke vina misimamo tofauti kuhusu masuala mengi kama vile katika siasa za nje,au sekta zinazohusika na fedha,jamii na uchumi. Amesema,tofauti hizo ni kubwa mno na kwa hivi sasa hakuna msingi wa kuweza kushirikiana kisiasa.

Licha ya kupoteza umaarufu wake miongoni mwa wanachama wa SPD,Kurt Beck amesema,yeye hafikirii kujiuzulu na kamwe hajuti kushika wadhifa wa mwenyekiti wa chama.Akaongezea kuwa mtu hakimbii shida,matatizo yanapoibuka.