1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha waziri mkuu aliepinduliwa chapata viti vingi bungeni Thailand

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CfkW

BANKOK:

Chama kinachohusiana na waziri mkuu alieondolewa madarakani Thaksin Shinawatra, kimeanza kutafuta washirika siku moja tu baada ya uchaguzi wa wabunge nchini Thailand.

Matokeo kamili yanatarajiwa jumatatu lakini chama cha Peoples Power Party-PPP kinaweza kikaibuka na viti 228 vya bunge. Ni kasoro ya viti 13 kuweza kupata wingi wa kura. Ushindi wa PPP ni kama kuulaumu utawala wa kijeshi ambao ulimuondoa madarakani Thaksin miezi 15 iliopita na tangu wakati huo jeshi limekuwa likajaribu kuzuia umaarufu wake.

Mkuu wa chama cha PPP-Samak Sundaravej amesema kuwa atamuomba Thanksin arejee nyumbani kutoka uhamishoni.Haijulikani ikiwa waziri mkuu huyo wa zamani anaweza kutoa mchango wowte wa kisiasa kwani amepigwa marufuku kutojihusisha katika siasa kwa kipindi cha miaka 5.