1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Champions League : Ronaldo kurejea Old Traford

20 Desemba 2012

Christiano Ronaldo atarejea na mabingwa mara tisa wa Champions League Real Madrid katika uwanja wa Old Traford kupambana na Manchester United ambako alijitokeza kuwa mshambuliaji hatari kabisa duniani.

https://p.dw.com/p/176Ve
ARCHIV - UEFA-Generalsekretär Gianni Infantino zieht am 20.07.2012 Lose bei der Auslosung für die Champions League in Nyon. Für sieben Bundesliga-Teams wird es am 20.12.2012 spannend: Sie bekommen bei der Auslosung in Nyon ihre Gegner für die nächste Runde in der Champions und Europa League. EPA/LAURENT GILLIERON +++(c) dpa - Bildfunk+++
Draw ya Champions League iliyofanyika mjini Nyon, Uswisi.Picha: picture-alliance/dpa

Bayern Munich , ambayo ilifanikiwa kuingia katika fainali ya michuano hiyo msimu uliopita na kuambulia patupu dhidi ya Chelsea , London, inapambana mara hii na Arsenal London na Juventus Turin inatiana kifuani na Celtic Glasgow. Paris St Germain ambayo imetumia fedha nyingi msimu huu kununua wachezaji inakabiliana na Valencia ya Uhispania.

ARCHIV - Munich's Bastian Schweinsteiger reacts during the penalty shoot-out during the UEFA Champions League soccer final between FC Bayern Munich and FC Chelsea at Fußball Arena München in Munich, Germany, 19 May 2012. Photo: Tobias Hase dpa (zu dpa Jahresrückblick vom 30.11.2012) +++(c) dpa - Bildfunk+++
Mchezaji wa Bayern München Bastian Schweinsteiger akitokwa na machozi baada ya mchezo na ChelseaPicha: picture-alliance/dpa

Lakini majaliwa ya vigogo viwili vya soka la Hispania katika upangaji wa timu zitakavyoshindana leo Alhamis katika makao makuu ya shirikisho la soka barani Ulaya UEFA , umewavutia wapenzi wengi wa soka na wote wamepambanishwa dhidi ya vilabu vikongwe vyenye uzoefu mkubwa katika soka la Ulaya.

Real Madrid , mabingwa wa sasa wa Uhispania , wamekuwa katika hali ya kukatisha tamaa katika ligi ya nchi hiyo msimu huu na wamemaliza wakiwa katika nafasi ya pili katika kundi lao na mabingwa wa Ujerumani Borussia Dortmund katika Champions League.

Real Madrid's coach Jose Mourinho from Portugal checks his watch during a training session at the Valdebebas stadium on the eve of a Champions League Group D soccer match against Manchester City, in Madrid, Monday, Sept. 17, 2012. (Foto:Daniel Ochoa De Olza/AP/dapd)
Kocha Jose Mourinho katika mazoezi ya Real MadridPicha: dapd

Ronaldo kurejea Old Traford

Lakini Ronaldo, mchezaji wa Manchester United kuanzia mwaka 2003 hadi 2009, atakuwa na hamasa kwa Real kufanya vizuri dhidi ya klabu ambayo alishinda medali ya dhahabu katika ubingwa wa Ulaya mwaka 2008.

Kocha wa Real Madrid , Jose Mourinho, ambaye aliwahi kuifunza Chelsea, pia atapambana na hasimu wake wa zamani Alex Ferguson.

Dortmunds Mario Götze (L) and Real Madrid's Cristiano Ronaldo vie for the ball during the Champions League Group D soccer match between Borussia Dortmund and Real Madrid at BVB Stadium Dortmund in Dortmund, Germany, 24 October 2012. Photo: Kevin Kurek/dpa
Mchezo wa kundi D katika ya Real na DortmundPicha: picture-alliance/dpa

"Nina hakika litakuwa pambano la pekee kwa Ronaldo" amesema Emilio Butragueno, mkurugenzi wa Real Madrid anayehusika na mahusiano ya taasisi.

"Nafikiri mashabiki watafurahi sana katika pambano hili la kufurahisha.

"Itakuwa kitu cha kufurahisha kwa kila mtu. Ningependa kucheza dhidi ya Manchester United katika sehemu za mwishoni mwa msimu huu wa champions league , lakini mashabiki wasingefurahi hata hivyo."

Manchester United mabingwa wa kombe hilo mara tatu, wamecheza na Real Madrid mara nane na kushinda mara mbili tu. Real , ambayo itaikaribisha Manchester katika mchezo wa kwanza Februari 13, iliweza kushinda mara ya mwisho kombe la Champions League mwaka 2002.

Barcelona inatisha

Barcelona hivi sasa wanapewa nafasi ya juu kulinyakua kombe hilo, licha ya kuwa wasingependa kukutana na timu yenye uzoefu mkubwa katika soka la Ulaya kama mabingwa mara saba wa kombe hilo AC Milan.

Mchezaji bora wa dunia Lionel Messi amepachika wavuni mabao 90 mwaka huu wa 2012 na ameiiwezesha Barcelona kuongoza ligi ya Uhispania kwa points tisa sasa kutoka timu inayofuatia wakati Milan wako points 14 nyuma ya Juventus Turin inayoongoza ligi ya Italia , Serie A.

epa03444072 FC Barcelona's Argentinian striker Lionel Messi (R) vies for the ball with Celtic Glasgow's captain Scott Brown (L) during their UEFA Champions League group G soccer match at Camp Nou in Barcelona, northeastern Spain, 23 October 2012. EPA/ALBERT OLIVE +++(c) dpa - Bildfunk+++
Messi akichanja mbuga katika mpambano na CelticPicha: picture-alliance/dpa

Bayern Munich timu iliyonyang'anywa tonge kinywani nyumbani na Chelsea msimu uliopita inaongoza kwa points tisa katika ligi ya Ujerumani , Bundesliga. Bayern imefurahi kupangwa na Arsenal ikifahamu kuwa wapinzani wao hao wanahangaika kujiweka sawa katika ligi ya Uingereza Premier League.

Mabingwa wa Ujerumani Borussia Dortmund hawajisikii nafuu kukumbana na mabingwa wa Ukraine Shakhtar Donetsk. Mwenyekiti wa Dortmund Hans Joachim Watzke amesema haikuwa timu ambayo tungependa kukumbana nayo wakati huu. Ni timu ngumu sana lakini tumeonyesha katika mtoano katika makundi kuwa tunaweza kushinda hata timu ngumu.

Dortmund's Julian Schieber (C) celebrates with his teammates Kevin Grosskreutz, Ivan Peresic and Felipe Santana after scoring the 1:0 during the UEFA Champions League group D soccer match between Borussia Dortmund and Manchester City at BVB stadium in Dortmund, Germany, 04 December 2012. Photo: Bernd Thissen/dpa
Kikosi cha BVB Borussia Dortmund wakirejea baada ya kuweka mpira wavuni kwa Man CityPicha: picture-alliance/dpa

Schalke 04 imepangwa dhidi ya Galatasaray ya Uturuki na Porto ya Ureno inapambana na Malaga ya Uhispania.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre

Mhariri: Yusuf Saumu