1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Changamoto zilizopo kuhusu nadharia ya hivi sasa za sera za kiusalama nchini Urusi.

Sekione Kitojo6 Julai 2009

Rais wa Marekani Barack Obama anaelekea nchini Urusi kwa mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo ambapo amekuwa akisisitiza juu ya kuwapo mtazamo mpya kuhusu usalama.

https://p.dw.com/p/Ihuf
Picha za kitamaduni za kuchonga za Urusi baadhi yake zikiwa katika sura ya rais Obama na Medvedev. zikiwa zimewekwa mjini Moscow.Picha: AP

Leo Jumatatu rais wa Marekani Barack Obama anawasili nchini Urusi, ambako kwa muda wa wiki chache zilizopita amekuwa akisisitiza kuwapo kwa mtazamo mpya juu ya suala la usalama. Sera za mambo ya kigeni zinachukua nafasi ya chini. Marekani na jumuiya ya NATO kwa Urusi zinabaki hata hivyo kuwa suala la uadui.


Urusi ilibidi kupambana na matokeo ya mzozo wa kisiasa na kiuchumi mwishoni mwa karne ya 20 , ndio sababu nchi hiyo ilianzisha kwa hali ya kujiamini , nadharia mpya ya kiusalama ambayo ilianzishwa na rais wa Urusi Dmitry Medvedev katikati ya mwezi Mei. Waraka huo una vipengee 116 vya tathmini na unapaswa kuwa mwongozo kwa sera za mambo ya ndani na ya kigeni kwa Urusi hadi mwaka 2020.

Kama anavyosema mwakilishi wa mkurugenzi wa baraza la urusi la masuala ya kigeni na sera za ulinzi, Dmitrij Suslov.

Kazi muhimu na wakati huo huo inayoweza kuipeleka mbele Urusi imo mikononi mwa nchi hiyo binafsi. Kwa hiyo kuna haja ya dharura ya kufanya mfumo wa kisasa zaidi utakaoweza kufanyakazi ya kuubadilisha mwelekeo wa taifa, na kupambana na ufisadi na mambo mengine.


Kwa mara ya kwanza katika historia ya hivi karibuni ya Urusi usalama wa nchi hiyo hautaendeshwa na masuala ya kigeni ama kubainishwa na uwezo wake wa kiulinzi. Hii ni hoja yenye mantiki, anasema mtaalamu wa Urusi katika shirika la Ujerumani kuhusu sera za mambo ya kigeni Alexander Rahr.

Changamoto kuhusiana na siasa za mambo ya ndani nchini Urusi hivi sasa ziko katika nafasi ya mbele kabisa. Ni jambo la kawaida , kwa kuwa uhusiano na mataifa ya magharibi katika wiki ama miezi iliyopita tangu kuingia madarakani kwa rais Barack Obama umekuwa bora zaidi.


Usalama wa taifa nchini Urusi uliotolewa katika waraka huo unaeleza wazi hususan suala la kuporomoka kwa uchumi pamoja na viwango vya kijamii. Na pia kuna masuala yaliyoangaliwa kwa karibu kama ukuaji wa uchumi, afya, sayansi, elimu, utamaduni na hali bora ya maisha. Hapa kuna lengo kuu muhimu lililowekwa, ambapo katika muda wa kati na pia kwa kuwa Urusi inataka kujitokeza mbele duniani kuhusiana na maeneo yenye matatizo. Tatizo kubwa kwa usalama wa taifa ni suala la ukosefu wa kazi, kupanda kwa mgawanyiko wa kijamii, kupungua kwa ongezeko la watu na kupanda kwa gharama za ndani.


Mwandishi: Nikita,Jolkver/DE Russisch (Berlin)/Sekione Kitojo

Mhariri:M.Abdul-Rahman