1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chelsea ndio mabingwa wa Uingereza

4 Mei 2015

Chelsea imejihakikishia ubingwa wa Premier League msimu huu nchini Uingereza ikiwa imebakia michezo mitatu baada ya ushindi wa kazi wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace

https://p.dw.com/p/1FJyz
England Chelsea Meister Jubel
Picha: Reuters/Recine Livepic

Kocha Jose Mourinho licha kukosolewa kwamba timu yake inacheza mchezo usio pendeza, amesema anajisikia vizuri kupata ubingwa wa Premier League.

Mourinho alisema "Ina maana , wakati ukIfanyakazi kwa nguvu zote na unakuwa bingwa unajisia umepata kile unachostahili. Hisia hizo nzuri kwangu mimi , huenda ni hisia maalum kwa sababu mimi sio mtu mwenye uwezo mzuri wa kuchangua nchi na vilabu. Naweza kuchagua klabu nyingine katika nchi nyingine ambako kuwa bingwa ni rahisi, lakini nimechagua ligi ambayo ni ngumu mno barani Ulaya. Nachagua klabu ambayo nilikuwa na furaha kabla. Nchini mwangu, tunasema mengi kuhusu kurejea kule ambako ulikuwa na furaha kabla kwa sababu unahatarisha kile ulichofanya kabla. Kwa hiyo nimejihatarisha na nina furaha sana , sana kwa sababu nimeshinda ubingwa wa Premier League.

Hata hivyo Mourinho anaamini kwamba msimu ujao utakuwa mgumu zaidi hata kupata nafasi nne za juu za Champions League kutokana na ushindani unaoongozeka katika ligi hiyo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / rtre / dpae /
Mhariri: Daniel Gakuba