1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chiellini: adhabu aliyopewa Suarez ni kali mno

27 Juni 2014

Beki wa Italia Giorgio Chiellini aliyeng'atwa begani na Luis Suarez amesema adhabu aliyopewa mshambuliaji huyo wa Uruguay ni kali mno. Suarez amewasili Uruguay baada ya kutimuliwa katika Kombe la Dunia

https://p.dw.com/p/1CRj4
Fifa WM Italien Uruguay Chiellini Bissspuren Suarez
Picha: picture-alliance/dpa

Chiellini amesema kwenye tovuti yake kwamba kila mara yeye huunga mkono hatua za kinidhamu zianzochukuliwa na mashirika husika, lakini wakati huo huo, anaamini kuwa mfumo uliotumiwa ni wa kupindukia.

Chiellini amesema amemhurumia Suarez pamoja na familia yake. Ameongeza kuwa anatumai Suarez ataruhusiwa kuwa karibu na wachezaji wenzake wakati wa mechi, kwa sababu hatua kama hiyo ya kupigwa marufuku inamtenga sana mchezaji.

Shirikisho la FIFA, lilimfungia mshambuliaji Luis Suarez kucheza michezo tisa ya kimataifa pamoja na kushiriki katika shughuli zozote zinazohusiana na mchezo wa soka kwa kipindi cha miezi minne

FIFA WM 2014 Suarez Fans auf dem Flughafen von Montevideo 26.06.2014
Mshabiki wa Suarez walimlaki katika uwanja wa ndege ili kumuunga mkono nyota waoPicha: Reuters

Kwa mujibu wa msemaji wa shirikisho la soka duniani FIFA, Delia Fischer adhabu ya Luis Suarez inaanza mara moja na mshambuliaji huyo ataukosa mchezo wa hatua ya 16 bora katik ya timu yake ya Uruguay na Colombia aidha anatarajiwa kukosa zaidi ya michezo 30 ya ligi kuu ya Uingereza kutokana na kufungiwa kushiriki katika matukio yoyote ya michezo ikiwemo kuingia viwanjani.

Wakati huo huo, mfuko wa nyota wa Uruguay Luis Suraz tayari umeanza kuathirika, baada ya mfadhili wake mkuu alipotangaza kuufuta mkataba wake maramoja, kwa kumng'ata mpinzani wake wa Italia Giorgio Chiellini tukio ambalo lilisababisha yeye kutimuliwa katika Kombe la Dunia.

Tovuti ya kuwekeana dau ya 888 ambayo iliingia mapatano na Suarez baada ya kuwa na msimu wenye mafanikio makubwa katika klabu yake ya Liverpool, lakini sasa imesitisha mahusiano yake na nyota huyo.

Hatua yao imefuatia ile ya kampuni kubwa ya Adidas, ambayo pia iliufuta ushiriki wa mchezaji huyo katika matangazo yake yote ya Kombe la Dunia, na ikasema itatathmini ushirikiano wao namchezaji huyo baada ya kukamilika Kombe la Dunia. Suarez aliondoka Brazil mara baada ya kupewa adhabu kali zaidi kuwahi kutolewa katika historia ya kinyng'anyiro hicho.

Mwisho wa habari za michezo kwa sasa, mimi ni Bruce Amani kutoka Bonn. Kwaheri

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman