1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China na Japan kuimarisha mahusiano ya kiuchumi

Lilian Mtono
26 Oktoba 2018

China pamoja na Japan kwa pamoja zimekubaliana kuimarisha uhusiano ya kiuchumi baina ya mataifa yao, katika wakati ambapo China iko kwenye mzozo mkali wa kibiashara na Marekani. 

https://p.dw.com/p/37EmN
Peking Treffen   Li Keqiang und Shinzo Abe
Picha: Reuters/R. Pilipey

Waziri Mkuu wa China Shinzo Abe pamoja na Waziri Mkuu wa Japan, Li Keqiang kwa pamoja wamekubaliana kuimarisha uhusiano ya kiuchumi baina ya mataifa yao, katika wakati ambapo China iko kwenye mzozo mkali wa kibiashara na Marekani. 

Kwenye hafla ya kutiliana saini makubaliano yaliyofikiwa baina ya viongozi hao wakati wa ziara ya waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe nchini China, alinukuliwa akisema ''Tumekubaliana pia kuendeleza kwa karibu ushirikiano na kutekeleza jukumu letu katika kufanikisha lengo letu la pamoja la kuondoa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea Kaskazini.''

Na waziri mkuu wa China Li Keqiang kwa upande wake alisema ''China na Japan ni majirani muhimu. Amani, urafiki na mashirikiano ni masuala ya msingi kwa pande zote. China na Japan ni mataifa muhimu barani Asia. Kuendeleza usalama wa kikanda na maendeleo ni majukumu ya msingi ya mataifa yetu mawili.''

Aidha, waziri mkuu Abe amesema Japan ina jukumu kubwa la kuhakikisha usalama wa kikanda na kuongeza kuwa mataifa hayo mawili yanatakiwa kurejesha  mahusiano yao katika hali ya kawaida na kushirikiana katika masuala yahusuyo Korea Kaskazini.

Japan Tokio Abflug Shinzo Abe nach China
Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe yuko ziarani nchini China.Picha: picture-alliance/Jiji Press/K. Sumiyoshi

Kulingana na shirika la habari la Kyodo, Waziri mkuu Abe ambaye yuko ziarani nchini China, amekubaliana na mwenzake Li Keqiang kushirikiana pia kwenye maeneo kama ya teknolojia ya kisasa na ulinzi wa haki miliki, lakini pia kurejesha biashara ya kubadilisha sarafu katika nyakati zinapotokea dharura za kifedha.

Waziri mkuu Abe, pia anatarajiwa kukutana na rais wa China, Xi Jin Ping, ambaye ameandaa chakula cha makaribisho cha mchana pamoja na dhifa ya kitaifa kwa kiongozi huyo. Hii ni ziara ya kwanza nchini China kufanywa na waziri mkuu wa Japan katika kipindi cha miaka saba.

Waziri mkuu Abe, pia anatarajiwa kukutana na rais wa China, Xi Jin Ping, ambaye ameandaa chakula cha makaribisho cha mchana pamoja na dhifa ya kitaifa kwa kiongozi huyo. Hii ni ziara ya kwanza nchini China kufanywa na waziri mkuu wa Japan katika kipindi cha miaka saba.

Abe na Xi  watajadiliana kwa upana kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa, ambayo ni pamoja na mpango wa kuondoa silaha za nyuklia Korea Kaskazini. Abe pia amemualika Xi kuitembelea Japan mwakani.

Kongamano kuhusu mashirikiano kati ya China na Japan litakalojadili masuala ya miundombinu kwenye nchi zinazoendelea linataraji kufanyika hii leo. China ni mshirika mkuu wa kibiashara wa Japan, na kiwango cha biashara kati yao kilifikia dola bilioni 300 mwaka jana.

Mwandishi: Lilian Mtono/DPAE/DW

Mhariri: Grace Patricia Kabogo