1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China kununua vinu vya kinuklia kutoka Ufaransa.

26 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTGI

Beijing. Shirika la Areva la Ufaransa limesema limepata mkataba wa Euro bilioni 8 wa kuuza vinu viwili vya kinuklia nchini China. Tangazo hilo ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa muda mrefu limekuja mwanzoni mwa mazungumzo rasmi mjini Beijing baina ya rais wa Ufaransa Nocolas Sarkozy na mwenzake wa China Hu Jintao. Makubaliano hayo yanatarajiwa kutiwa saini katika sherehe baadaye leo.Rais Sarkozy ameanza ziara yake ya siku tatu nchini China jana Jumapili kwa kutoa wito kwa China kuiachia sarafu yake ya Yuan kupanda. Kumekuwa na hali ya wasi wasi katika bara la Ulaya katika miezi ya hivi karibuni juu ya athari mbaya ambayo sarafu ya Euro inayozidi kupanda inaweza kuna nayo katika mauzo ya bidhaa nje.