1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaionya Taiwan juu ya kujiamulia hatma yake ya kisiasa

5 Machi 2008

-

https://p.dw.com/p/DIEf

BEIJING

Waziri mkuu wa China Wen Jiabao ameionya Taiwan leo hii juu ya kujiamulia peke yake kuhusu hatma yake ya kisiasa wakati kisiwa hicho kilichojitenga kikijiandaa na kura ya maoni juu ya ikiwa kitafute uanachama katika Umoja wa Mataifa.

Kisiwa hicho ambacho China inadai ni chake kinatazamiwa kupiga kura ya maoni pamoja na uchaguzi wa rais tarehe 22 mwezi huu hatua ambayo inaonekana kupuuza maonyo yaliyotolewa na Marekani,Ufaransa,Japan na China.Ikiwa kura hiyo ya maoni itapita huenda ikaangaliwa na China ambayo ni mwanachama mwenye kura ya turufu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataiafa kama ni tangazo rasmi la kisiwa hicho kwamba kimejitangazia uhuru .Hapo jana rais wa China Hu Jintao aliitaka Tiawan kurudi kwenye meza ya mazungumzo chini ya mwito wa sera ya moja ya China lakini kisiwa hicho kinapinga sera hiyo ambayo imeitaja kuwa isiyokuwa na haki.Mazungumzo yalikwama tangu mwaka 199 wakati rais wa Taiwan Lee Teng Hui aliposisitiza kwamba uhusiano wa masuala ya kibishara yafanyika kati ya nchi na nchi jambo ambalo serikali ya China inasema itaamisha kisiwa hicho ni nchi kivyake.