1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yamfunga mwanasayansi aliyerekebisha vinasaba

30 Desemba 2019

Mahakama nchini China imemuhukumu kifungo cha miaka 3 jela mwanasayansi mmoja aliyejitapa kufanikisha kuzaliwa kwa watoto wa kwanza duniani ambao vinasaba vyao vimefanyiwa marekebisho.

https://p.dw.com/p/3VVtt
He Jiankui | China Forschung
Mwanasayansi He Jiankui,Picha: Imago Images/ZUMA Press/S.C. Leung

Mahakama ya nchini China imemuhukumu kifungo cha miaka 3  jela mwanasansi mmoja aliyejitapa kufanikisha kuzaliwa kwa watoto wa kwanza ambao vinasaba vyao vimefanyiwa marekebisho kitendo kilichotajwa kuwa ni kinyumecha sheria katika fani ya utabibu.

He Jiankui ambaye mwaka uliopita aliiistaajabisha jumuiya ya wanasayansi duniani kwa kutangaza kuzaliwa mapacha wa kike ambao vinasaba vyao vilifanyiwa marekebisho ili kutoa kinga ya kuzuiwa uwezekano wa kushambuliwa na virusi vya ukimwi, pia amepigwa faini ya dola 430,000 .

Jiankui  aliyepata elimu kutoka chuo kikuu cha Stanford amehukumiwa na mahakama ya mji wa Shenzhen kwa kufanya matendo yaliyo kinyume cha sheria dhidi ya vinasaba vya kiinitete cha binadamu kilichohifadhi kwa ajili ya majaribio yanayokubalika na sheria za kitabibu.

Watafiti wengine wawali walioshrikiana naye pia wamehukumiwa na mahakama hiyo.

Zhang Renli amehukumiwa kifungo cha miaka miwili na faini ya Yuan milioni moja wakati Qin Jinzhou amehukumiwa miezi 18 na kupigwa marufuku kwa miaka miwili kushiriki shughuli za kitabibu pamoja na kulipa faini ya Yuan 500,000.

Hawakutimiza vigezo vya kufanya kazi za utabibu 

CRISPR
Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Schiefelbein

Kulingana na shirika la habari la Xinhua watatu hao hawakuwahi kupata sifa za kufanya kazi kama madaktari na walifahamu kuwa wanakiuka kanuni na maadili ya utabibu ya China.

Walifanya hayo ´´katika kutafuta umaarufu na manufaa binafsi´´ imesema sehemu ya hukumu dhidi yao.

Watafiti hao walitengeneza kibali bandia cha tathmini ya maadili kabla ya kuwatafuta wanandoa ambao mwanaume alikuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa ajili ya utafiti wao.

Kesi yao iliendeshwa kwa kificho chini ya hoja ya haki ya faragha.

Majaribio ya kufanyia marekebisho vinasaba yalisababisha kutokea kwa mimba mbili ikiwemo moja ya mapacha walifanikiwa kuzaliwa na nyingine ya mtoto wa tatu ambaye hapo kabla kuzaliwa kwake hakukuthibitishwa.

Mafanikio yake yaliushangaza ulimwengu

China Forschung l He Jiankui - Drei Jahre Gefängnis für Genforscher
Picha: picture alliance/dpa/G. Fischer

Novemba mwaka uliopita Jiankui alitangaza kuzaliwa kwa watoto hao wa kwanza ambao vinisaba vyao vimefanyiwa marekebisho baada ya kufanikiwa kivifanya kuwa na kinga ya kuvizia kushambuliwa na virusi vya Ukimwi chini ya mbinu ya kisayansi iiwayo CRISPR.

Siku chache baadae Jiankui, Profesa wa zamani wa chuo kikuu cha sayansi na teknolojia mjini Shenzhen aliuambia mkutano wa masuala ya tiba mjini Hong Kong kwamba alihisi fahari kutokana na kazi aliyoifanya.

Tambo zake ziliistua jumuiya ya wanasayansi duniani na kuzusha maswali kuhusu maadili katika fani ya tiba na kumulika pia usimamizi dhaifu wa China katika tafiti za kisayansi.

Ufanyaji marekebisho katika vinasaba vya binadamu ni kinyume cha sheria kinyume cha sheria kwenye mataifa mengi.

Wizara ya afya ya China ilichapisha kanuni mpya mwaka 2003 kuzuia marekebisho kwenye vinasaba isipokuwa kwa matumzii yasiyohusu uzalishaji wa viumbe hai.