1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yapendekeza mpango mpya kwa Syria

Sekione Kitojo1 Novemba 2012

China imesema leo(01.11.2012)kuwa imependekeza mpango mpya utakaoweza kuzuwia ghasia nchini Syria,ikiwa ni pamoja na usitishaji wa mapigano kwa awamu kutoka jimbo hadi jimbo na kuanzisha chombo cha serikali ya mpito.

https://p.dw.com/p/16b44
The U.N.-Arab League envoy to Syria Lakhdar Brahimi, left, talks with Chinese Foreign Minister Yang Jiechi, right, during their meeting at the Ministry of Foreign Affairs in Beijing, China Wednesday, Oct. 31, 2012. Brahimi met Yang to solicit support from Beijing in international efforts to ending Syria's civil war. (Foto:Takuro Yabe, Pool/AP/dapd)
Lakhdar Brahimi akizungumza na viongozi nchini ChinaPicha: dapd

China imekuwa ikishutumiwa vikali na baadhi ya watu katika mataifa ya Kiarabu kwa kushindwa kuchukua msimamo imara kuhusiana na ghasia nchini Syria na imekuwa tu na nia ya kujaribu kuonesha kuwa inachukua jukumu la kutatua mzozo huo.

Mpango huo wa China, ulipendekezwa jana Jumatano(31.10.2012) kwa mjumbe wa jumuiya ya mataifa ya Kiarabu , Arab League na umoja wa mataifa Lakhdar Brahimi ambaye yuko katika ziara nchini humo, unakuja baada ya kuvunjika kwa pendekezo la hivi karibuni la kusitisha mapigano katika muda wa sikukuu ya Kiislamu ya Eid al-Adha.

The U.N.-Arab League envoy to Syria Lakhdar Brahimi talks with Chinese Foreign Minister Yang Jiechi, unseen, during their meeting at the Ministry of Foreign Affairs in Beijing, China Wednesday, Oct. 31, 2012. Brahimi met Yang to solicit support from Beijing in international efforts to ending Syria's civil war. (Foto:Takuro Yabe, Pool/AP/dapd)
Lakhdar BrahimiPicha: dapd

Mzozo huo ambao umedumu sasa kwa muda wa miezi 19, ambapo waasi wanajaribu kuuondoa utawala wa rais Bashar al-Assad, umesababisha vifo vya zaidi ya watu 32,000 hadi sasa.

Usitishaji mapigano awamu kwa awamu

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya China Hong Lei amesema katika mkutano na waandishi habari kuwa chini ya pendekezo hilo jipya kuna ushauri kadha mwingine muhimu kama vile usitishaji wa mapigano jimbo kwa jimbo na awamu kwa awamu, na kuundwa kwa chombo kitakachochukua madaraka ya kuiongoza nchi hiyo kwa misingi ya mpito.

Wakati huo huo kiongozi wa kundi kuu la upinzani nchini Syria , baraza la taifa nchini humo, leo ameilaumu jumuiya ya kimataifa kwa kushindwa kuchukua hatua katika mzozo nchini humo na kusababisha kuchochea hisia za kidini kwa Waislamu wenye imani kali.

Matamshi hayo yamekuja siku moja baada ya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton kusema kuwa upinzani nchini Syria unapaswa kuzuwia kwa njia zote juhudi za Waislamu wenye imani kali kuteka mapinduzi nchini Syria.

U.S. Secretary of State Hillary Clinton winks after addressing an event to discuss leveraging AIDS response during the 67th United Nations General Assembly at the U.N. Headquarters in New York, September 26, 2012. REUTERS/Lucas Jackson (UNITED STATES - Tags: POLITICS TPX IMAGES OF THE DAY HEALTH)
Hillary ClintonPicha: Reuters

Jumuiya ya kimataifa haifanyi lolote Syria

Akizungumza kwa njia ya simu kutokea nchini Uturuki, mwenyekiti wa baraza la taifa SNC Abdel Basset Sayda amesema kuwa hali hiyo imetokana na jumuiya ya kimataifa kutofanya chochote nchini Syria.

A leader of the Syrian National Council (SNC), Abdulbaset Sieda meets with Russian Foreign Minister Sergey Lavrov, not pictured, in Moscow, Russia, Wednesday, July 11, 2012. (Foto:Misha Japaridze/AP/dapd).
Kiongozi wa baraza la taifa la Syria Abdulbasset SaydaPicha: dapd

Wakati huo huo waasi wamewauwa wanajeshi 28 wa jeshi la serikali leo katika shambulio dhidi ya vituo vitatu vya upekuzi barabarani karibu na mji wa Saraqeb, ambao uko katikati ya barabara kuu upande wa kusini kaskazini, kundi moja linalofungamana na upinzani limesema.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / rtre

Mhariri: Mohammed Khelef