1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kuhusu mazingira wa Bali

Siraj Kalyango7 Desemba 2007

Marekani na Saudi Arabia namba moja kwa uchafuzi wa maziingira

https://p.dw.com/p/CYej
Mtetezi wa mazingira akivaa nguo ya Dubu akiwa karibu na kipimi bandia cha hali joto nje ya mkutano wa BaliPicha: AP

Mkutano kuhusu hali ya joto duniani unaofanyika Indonesia umeisifu China katika juhudi zake kuunga mkono hatua za kupinga kuongezeka kwa hali ya joto duniani.

Huku Marekani na Saudi Arabia kulaumiwa kuwa mstari wa mbele kuchafua mazingira.

Baadhi ya watalaam wanasema China imeipiku Marekani kama mchafuzi wa mazira duniani.Hii inatokana na kukua kwa haraka kwa uchumi wake.Viwanda vinachipuka kila kukicha na hivyo kuchafua mazingira kwa fujo.

Lakini kinyume na ilivyotarajiwa kabla ya mkutano wa hali ya hewa wa Bali nchini Indonesia, badala yake umeisifu China kuhusu hali ya hewa.Marekani kwa upande wake imelaumiwa kwa kejeli yake.

China imesifiwa kutokana na juhudi zake za kuunga mkono vita dhidi ya kuongezeka kwa hali joto duniani.

Mmoja wa wajumbe katika mkutano huo kutoka tume ya Ulaya, Arthur Runge- Metzger, amenukuliwa kusema kuwa, anafikiri kuwa china inachukulia suala la hali ya hewa kwa makini na hivyo hiyo ni alama nzuri na yaweza kuzalisha matokeo bora katika mkutano huo.

Sasa Marekani na Saudi Arabia ndio zimegunduliwa kama nchi ambazo ziko mstari wa mbele kuchafua mazingira.

Makundi yanayotetea mazingira yametoa vigezo kwa nchi 56 zenye viwanda vingi pamoja na zile zinazonukia. Sweden imechukua nafasi ya kwanza kama nchi isiochafua mazingira.

Hata hivyo imepata alama ndogo.China imepanda juu katika nafasi ya nne kutoka kutoka ile ya mwaka jana. Mwaka uliopita ilikuwa ya 43 na sasa ni ya 40.

Saudi Arabia ambayo ndio inaongoza kuuza mafuta duniani, imekuwa ya mwisho katika orodha ya nchi zinachafua mazingira.

Saudi Arabia imeshikilia nafasi hiyo ya chini kwa mara ya pili mfululizo.Hii ni kutokana na sera zake za kutilia munda juhudi za kuzuia uchafuzi wa mazingira.

Marekani inaishinda alama moja tu.

Marekani ndio nchi pekee ilioendelea kiviwanda ambayo haijatia sahihi mkataba wa Kyoto.

Marekani kama nchi zingine zenye viwanda inaogopoa kutia sahihi mkataba wa Kyoto kutokana na hofu ya kuathiri uchumi wake.

Mkurugenzi wa shirika la umoja wa mataifa la mazingira-UNEP, Janos Pasztor, ameondoa hofu hiyo akisema kuna nafasi kubwa ya kuwepo kwa kazi zinazoheshimu mazingira na zitaweza kuleta faida kwa wahusika wote.

Watafiti pamoja na wanamazingira jana , katika mkutano wa Bali, kinyume na kawaida yao walijiunga katika ulingo wa kisiasa kuhusiana na hali ya hewa.

Wametoa mwito wa kuwekwa kiwango cha asili 50 ya kuwa ndio bora cha kutoa gesi aina ya kaboni ifikapo mwaka wa 2050.Wataalamu hao kawaida hutoa tu utafiti wao na kuwaachia wanasiasa kuchua mwelekeo waupendao. Licha ya Marekani kushihinikizwa baado ilikataa kukubali.