1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yataka ushirikiano wa kijeshi na Syria

Admin.WagnerD16 Agosti 2016

China inataka kuwa na uhusiano wa karibu wa kijeshi na Syria wakati Urusi ikiitumia Iran kama kambi ya kufanya mashambulizi yake ya anga dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali nchini Syria kwa mara ya kwanza.

https://p.dw.com/p/1JjH5
Picha: Reuters

China inataka kuwa na uhusiano wa karibu wa kijeshi na Syria hayo yamebainika kufuatia ziara ya aina yake iliofanywa na afisa mwandamizi wa serikali ya China katika nchi hiyo iliokumbwa na vita Mashariki ya Kati na wakati Urusi ikiitumia Iran kama kambi ya kufanya mashambulizi yake ya anga dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali nchini Syria kwa mara ya kwanza leo hii. Mohamed Dahman na taarifa

Wakati China ikitegemea Mashariki ya Kati kwa ajili ya usambazaji wa mafuta nchi hiyo hupendelea kuliacha suala la diplomasia kwa eneo hilo kwa nchi nyengine wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa za Marekani, Uingereza na Ufaransa.

Hata hiyo nchi hiyo imekuwa ikijaribu kujihusisha zaidi ikiwa ni pamoja na kuwatuma wajumbe wake kusaidia kushinikiza utatuzi wa kidiplomasia kwa mzozo huo pamoja na kuwakaribisha nchini China viongozi wa serikali ya Syria na wale wa upizani

Kwa mujibu wa shirika la habari la China Xinhua mkurugenzi wa ofisi ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Kijeshi katika Kamati Kuu ya Kijeshi nchini China Guan Youfei amekutana na waziri wa ulinzi wa Syria Fahad Jassim al- Freij mjini Damascus.

Dhima chanya ya China

Guan amesema China daima imekua ikitimiza dhima chanya katika kushinikiza utatuzi wa kisiasa nchini Syria.Shirika hilo la habari la China limemkariri afisa huyo akisema jeshi la China na la Syria yamekuwa na uhirikiano wa kirafiki wa jadi na kwamba China iko tayari kuendelea kubadilishana mawazo na ushikiano na jeshi la Syria.

China inataka kuwa na uhusiano wa karibu wa kijeshi na Syria hayo yamebainika kufuatia ziara ya aina yake iliofanywa na afisa mwandamizi wa serikali ya China katika nchi hiyo iliokumbwa na vita Mashariki ya Kati na wakati Urusi ikiitumia Iran kama kambi ya kufanya mashambulizi yake ya anga dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali nchini Syria kwa mara ya kwanza leo hii.
China inataka kuwa na uhusiano wa karibu wa kijeshi na Syria hayo yamebainika kufuatia ziara ya aina yake iliofanywa na afisa mwandamizi wa serikali ya China katika nchi hiyo iliokumbwa na vita Mashariki ya Kati na wakati Urusi ikiitumia Iran kama kambi ya kufanya mashambulizi yake ya anga dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali nchini Syria kwa mara ya kwanza leo hii.Picha: picture-alliance/dpa/Russian Defence Ministry

Bila ya kufafanua shirika hilo la Xinhua limesema pande zote mbili zimezungumzia juu ya mafunzo ya kijeshi na zimefikia muafaka kwa jeshi la China kuipatia Syria msaada wa kibinaadamu.

Wakati China haikonyesha utashi wa kujihusisha kijeshi nchini Syria mjumbe maalum wa nchi hiyo kwa mzozo wa Syria hapo mwezi wa Aprili alipongeza dhima ya kijeshi ya Urusi katika vita hivyo.

Wasi wasi wa Umoja Mataifa

Umoja wa Mataifa umesema leo hii una wasi wasi mkubwa kwa usalama wa raia katika mji wa Allepo wakati vikosi vya serikali na waasi vikizidisha mashambulzi yao.

Hali ya mji wa Aleppo kufuatia mapigano yanayoendelea.
Hali ya mji wa Aleppo kufuatia mapigano yanayoendelea.Picha: picture alliance/AA/I. Ebu Leys

Alessandra Velluccin msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema "Tume ya Umoja wa Mataifa ina wasi wasi mkubwa kwa usalama wa raia wakiwemo watoto 100,000 wanaoishi mashariki mwa mji wa Aleppo ambapo matumizi ya nguvu yamefikia kiwango cha juu kabisa katika wiki za hivi karibuni wakati mapambano yakipamba moto kuwania udhibiti wa vitongoji vinavyoshikiliwa na waasi na njia kuu zilizobakia za kusafirisha mahitaji."

Urusi leo imeitumia Iran kama kambi ya kufanyia mashambulizi yake ya anga dhidi ya wanamgambo nchini Syria.Hii ni mara ya kwanza kwa Urusi kutumia ardhi ya nchi nyengine mbali na Syria yenyewe kufanya mashambulizi ya aina hiyo tokea Kremlin Ikulu ya Urusi ilipoanzisha kampeni hiyo ya mashambulizi ya anga kumsaidia Rais Bashar al- Assad hapo mwezi wa Septemba.

Mwandishi : Mohamed Dahman

Reuters/AFP

Mhariri : Daniel Gakuba