1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chissano awasili Uganda

Aboubakary Liongo13 Desemba 2007

Rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chissano amewasili nchini Uganda katika jitihada za kuupa uhai mpango wa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

https://p.dw.com/p/CbIB
Joaquim Chissano
Joaquim ChissanoPicha: AP

Chissano ambaye ni mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, katika mzozo wa Kaskazini mwa Uganda anatarajiwa kukutana na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda na Joseph Kabila wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobini imesema kuwa Joachim Chissano anatarajiwa kuelekea mjini Juba kusini mwa Sudan ambako atakutana na wapatanishi pamoja na viongozi wa kundi la Lords Resistance Army.

Mazungumzo kati ya serikali ya Uganda na waasi wa LRA yameshindwa kufanyika toka yalipoahirishwa rasmi mwezi Mei mwaka huu.

Kiongozi huyo wa zamani wa Msumbiji mwezi uliyopita alikuwa mjini Kampala kwa majadiliano na maafisa wa serikali, na ingawaje hakuna tarehe rasmi iliyotajwa lakini, huenda pande mbili hizo zikarejea tena katika meza ya mazungumzo mwisho mwa mwezi huu au mapema mwezi ujayo.

Pamoja na kutiwa saini kwa mkataba wa kusitisha mapigano mwezi August mwaka jana, mabishano kati ya pande hizo mbili yamekuwa yakizidisha hofu ya kuvunjika kwa makubaliano hayo na wapiganaji wengi wa waasi hao wamekimbilia mafichoni katika maeneo ya kusini mwa Sudan na Kaskazini mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Kwa sasa ujumbe wa kiraia wa kundi hilo la LRA unafanya ziara katika eneo hilo lenye mzozo la kaskazini kukusanya maoni ya wananchi juu ya masuala ya uwajibikaji na maridhiano katika mazungumzo ya amani, ambavyo ni vitu muhimu katikia kumaliza mzozo huo.

Katika miezi ya hivi karibuni kundi hilo la LRA limekuwa likikabiliwa na hali mbaya ambapo baadhi ya makamanda wake wa juu wamejisalimisha kwa majeshi ya serikali na kupewa msamaha.

Pia majaaliwa ya Naibu Mkuu wa kundi hilo, Vicent Otti yakiwa hayajulikani, kufuatia habari ya kwamba aliuawa na mkuu wa kundi hilo, Joseph Kony madai ambayo yalipingwa.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ambayo imewatia hatiani makamanda watano wa kundi hilo akiwemo mkuu wao Josephy Kony na Otti imekataa kuondoa amri hiyo pamoja na wito kutoka kwa viongozi wa kundi hilo na babadhi ya maafisa wa serikali ya Uganda.

Kony amesema kuwa kamwe hatosaini mkataba wowote wa amani mpaka amri hiyo ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu, imeondolewa.

Kundi la LRA linatuhumiwa kwa kuendesha vitendo vya kinyama,vikiwemo, kubaka, kutesa , kuua raia, na kutumia watoto katika .

Mzozo katika eneo hilo la kaskazini mwa Sudan umeyagharimu maisha ya maelfu ya watu huku wengine kiasi cha millioni 2 wakiwa hawana makazi.

Kundi la LRA hapo mwanzo lilidai kuwa linapigana kutaka kuanzishwa kwa serikali itakayofuata misingi ya bibilia , lakini sasa limekubalia kukaka katika meza ya mazungumzo na serikali kuzungumzia masuala ya uchumi na kisissa.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameliomba Baraza la Usalama la Umoja huo kumuongezea muda Joachim Chissano katika jukumu lake la kusuluhisha mzozo huo wa kaskazini mwa Uganda.

Muda war ais huyo wa zamani wa Msumbuji kuwa mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa katika mzozo huo unamalizika mwaka huu.

Ban Ki-moon ameliomba Baraza hilo la Usalama kumongezea muda Chissano hadi Decemba mwakani.