1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Colombo.Ndege za jeshi la serikali zashambulia maeneo ya waasi.

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1u

Ndege za kijeshi za Sri Lanka zimeshambulia maeneo ya waasi wa Kitamil huko kaskazini mashariki mwa kisiwa hicho kufuatia shambulio la jana lililopelekea kuuwawa kwa watu 103, wengi wao wakiwa ni mabaharia.

Jeshi la nchi hiyo limesema,ndege za kijeshi zimeshambulia makao makuu ya waasi, huku waasi wakidai kuuwawa kwa wanakijiji wawili wa kike.

Kati ya sehemu zilizoripuliwa hapo jana kufuatia shambulio hilo ni pamoja na msafara wa mabasi uliokuwa ukisubiri kubeba wanamaji ambapo pia watu kiasi cha 150 walijeruhiwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan amelilaani shambulio la jana la kujitolea muhanga.