1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Comoro:Maandamano dhidi ya Ufaransa

28 Machi 2008

Wacomoro tangu Mayotte hata Ngazija waandamana dhidi ya Ufaransa kudai Col.Bacar arejeshwe huko.

https://p.dw.com/p/DWTD

Kiongozi-muasi wa kisiwa cha Comoro cha Nzouani,Mohammed Bacar,amewasilishiwa mapema leo kisiwani Reunion,kisiwa kiliopo ndani ya mamlaka ya Ufaransa kutokea Mayotte-mojawapo wa visiwa 4 vilivyounda Comoro kabla ya uhuru 1975.Serikali ya Comoro mjini Moroni inaendelea kudai Bacar arejeshwe Comoro kukabili mashtaka.Waandamnaji wenye hasira kutoka Nzouani waliandamana majiani mjini Mamoudzou,mji mkuu wa Mayotte kupinga kukimbilia huko kwa kanali Bacar.Ramadhan Ali na ripoti zaidi:

Col.Mohamed Bacar alisafirishwa kwa ndege mapema leo na wanajeshi wake 23 waasi wa kizouani hadi kisiwa jirani cha Reunion,milki ya Ufaransa katika Bahari ya Hindi.

Serikali ya Ufaransa imedai inamchunguza Bacar kwa kosa la kuingia Mayotte,kisiwa cha 4 cha Comoro,kinachodhibitiwa bado na Ufaransa - na silaha na bila ruhusa.Wakati huo huo,Ufaransa inazingatia ombo la Col.Bacar la hifadhi ya kisiasa.

Serikali ya Comoro, mjini Moroni, kisiwani Ngazija,inaendelea kudai Ufaransa imrudishe Col.Bacar akabili mashtaka.

Naibu waziri wa nje Houmadi Abdallah amewaambia maripota na ninamnukulu,

"Tumewakumbusha wafaransa kuwa hatia ya kimataifa ya kumtia yeye na wenzake ingali inafanya kazi."

Chama kinachotetea haki za binadamu cha Comoro halkadhalika, kimeitaka Ufaransa kumrejesha Col.Bacar Comoro.

Waziri mdogo wa milki za n'gambo wa Ufaransa, Yves Jego, anasema Ufaransa inazingatia ombi la Col.Bacar la hifadhi ya kisiasa na anatumai jibu litatolewa haraka iwezekanavyo.

kiroja cha mambo,ni kuwa Ufaransa pamoja na Marekani ikiungamkono opresheni ilioongozwa na vikosi vya Comoro vikisaidiwa na vya Umoja wa Afrika -Tanzania na Sudan kumtimua Bacar madarakani kisiwani Nzouani.

Baadhi ya wacomoro wanaituhumu Ufaransa kuwa nyuma ya kiongozi - muasi na kwamba eti imesaidia hata kutorokea kwake Mayotte.

Kabla kusafirishwa Bacar leo kutoka Mayotte hadi Reunion,vikosi vya ulinzi vya Ufaransa, viliweka ulinzi mkali uwanja wa ndege wa Pamandzi,Mayotte ambako Bacar alipelekwa kwa safari yake ya Reunion.Waandamanaji kutoka Nzouani huko Mayotte wakayapiga mawe magari ya wafaransa na wafaransa 2 wamejeruhiwa.Wamesema wamekasirishwa mno na hifadhi wafaransa wanayotoa muasi M.Bacar.

Mayotte binafsi ilikua mojawapo ya visiwa 4 vya Comoro kabla vitatu kujitangazia uhuru 1975.

Maandamano makali yalifanyika jana mjini Moroni,kisiwani Ngazija.Vikosi vya Umoja wa Afrika na vya jeshi dogo la Comoro vikamwaya hewa ya kutoa machozi kutawanya kundi la waandamanaji waliobeba mabiramu yalioilaani Ufaransa kuwa ni adui wa Comoro.

Maandamano halkadhalika, yalifanyika mbele ya Banki kuu ya Comoro ambako wafaransa wengi wanafanya kazina hata mbele ya Ubalozi wa Ufaransa.Huko waandamanaji walidai balozi wa Ufaransa afukuzwe nchini.Mwalimu mmoja wa kifaransa alijeruhiwa kidogo.

Wacomoro wangali na hasira kwamba ,mkuu wa majeshi ya askari wa kukodiwa walioivamia Comoro si chini ya mara 4 -mfaransa Bob- Denard, hakuhukumiwa ipasavyo kabla kufariki kwake.Bob Denard akiadi njama zake zote 4 huko Comoro zikiungwamkono na idara za ujasusi za Ufaransa.