1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CONAKRY : Bunge lakataa kurefusha sheria ya kijeshi

24 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPB

Bunge la Guinea hapo jana limekataa ombi kutoka kwa Rais Lansana Conte kuongeza muda wa sheria ya kijeshi katika hatua ya nadra ya ukaidi dhidi ya utawala wake wa kiimla.

Muda wa sheria hiyo ya kijeshi iliowekwa nchini kote siku 11 zilizopita kuzima maandamano ya ghasia yalioandamana na mgomo wa taifa ulikuwa ukitazamiwa kumalizika hapo jana lakini rais amelitaka bunge la taifa kurefusha sheria hiyo kutokana na wasi wasi wa usalama.

Hii inamaanisha kwamba hatua za sheria hiyo ya kijeshi ambayo imewapa jeshi madaraka makubwa ya kupekua na kukamata watu na kuweka amri ya kutotembea nje kuanzia jioni hadi alfajiri itakuwa imegoma kufanya kazi usiku wa manane wa hapo jana.

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wamekuwa wakidai kuwa Conte hafai kuongoza nchi na wamekuwa wakimtaka amchaguwe waziri mkuu mpya asiependelea upande wowote akiwa na madaraka kamili ya kuwateuwa na kuwatimuwa mawaziri wake.