1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CONAKRY : Kiongozi wa Guinea ateuwa waziri mkuu

10 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTe

Rais anayepigwa vita wa Guinea Lansane Conte hapo jana amemteuwa waziri mkuu mpya kutimiza ahadi aliyoitowa kufuatia mgomo wa taifa wa siku 18 uliopelekea kuuwawa kwa watu 59.

Hatua yake hiyo imekuja masaa machache tu baada ya ghasia mpya kuitingisha nchi hiyo.

Hata hivyo upinzani kwa haraka umepinga kuteuliwa kwa Eugene Camara mwenye umri wa miaka 64 waziri wa serikali wa muda mrefu kwa kile wanachosema kuwa ni mtu wa karibu mno kwa rais.

Wakati muda wa mwisho wa usiku wa manane wa Jumapili uliowekwa na vyama vya wafanyakazi unaomtaka rais kuchukuwa hatua hiyo venginevyo awe tayari kukabiliana na machafuko zaidi ukiwa unayoyoma kwa haraka maelfu ya waandamanaji hapo jana walifanya fujo kaskazini na magharibi ya nchi hiyo wakidai kujiuzulu kwa Conte ambaye ni mgonjwa.