1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Condolezza Rice kutia msukumo mazungumzo ya amani

5 Machi 2008

-

https://p.dw.com/p/DIEh

JERUSALEM

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice anakamilisha leo hii ziara yake ya siku mbili mashariki ya kati ambapo anatazamiwa kuwatia msukumo waisrael na wapalestina kurudi kwenye meza ya mazungo na kukomesha ghasia katika eneo la Ukanda wa Gaza linalodhibitiwa na chama cha Hamas.

Wanajeshi wa Israel walipambana tena na wanamgambo wa kipalestina kwenye eneo hilo.Vifaru na helikopta za kijeshi za Israeli zilishambulia nyumba karibu na mji wa kusini wa Khan Younis na kwa mujibu wa duru za hospitali mtoto mmoja aliuwawa kwenye mapigano hayo mapya.Uvamizi huo ulifanyika wakati Condolezza Rice alipokuwa akizungumza na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert mjini Jerusalem hapo jana.

Awali alisema kwamba wanamgambo wakipalestina lazima wakomeshe mashambulio ya roketi dhidi ya Israel na pia aliitaka Israel kutambua matokeo ya opresheni yake ya Kijeshi dhidi ya raia wasio na hatia Ukanda wa Gaza.