1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Confederations Cup: Fainali ni Brazil na Uhispania

28 Juni 2013

Baada ya Brazil, kukata tikiti ya fainali ya FIFA Confederations Cup hapo Jumatano, jana(27.06.2013) ilikuwa zamu ya mabingwa wa dunia na Ulaya Uhispania, kwa ushindi wa penalti dhidi ya Italia kwa mabao 7-6.

https://p.dw.com/p/18xkJ
epa03763647 Spanish National soccer team defender Alvaro Arbeloa (R) fights for the ball with midfielder Daniele De Rossi (L) of Italy during the FIFA Confederations Cup semi final match between Italy and Spain played at Castelao stadium in Fortaleza, Brazil, 27 June 2013. EPA/FELIPE TRUEBA +++(c) dpa - Bildfunk+++
FIFA Confederations Cup 2013Picha: picture-alliance/dpa

Jesus Navas alipachika bao muhimu baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kufungana katika dakika za kawaida pamoja na zile za nyongeza katika nusu fainali ya kombe la mabara, Confederations Cup.

Hakuna aliyekosa kutikisa wavu katika mikwaju ya penalti hadi pale mlinzi wa Italia Leonardo Bonucci alipoupaisha mkwaju wake juu ya goli na kumpa Navas kujaribu kuivukisha Uhispania katika kikwazo hicho.

epa03763695 Leonardo Banucci (C) of Italy and Daniele De Rossi (R) of Italy react next to goalkeeper Iker Casillas (L) of Spain during the Confederations Cup semi final match between Spain and Italy at the Castelao stadium in Fortaleza, Brazil, 27 June 2013. EPA/OLIVER WEIKEN
wachezaji wa Italia wakisikitika baada ya kukosa penaltiPicha: picture-alliance/dpa

Jesus Navas ambaye ametia saini hivi karibuni kuichezea Manchester City msimu ujao bila wasi wasi aliupachika mpira wavuni na kuivusha Uhispania hadi katika fainali ya mwaka huu ya kombe hilo la mabara.

Kocha akiri

"Tulikuwa na bahati katika mikwaju ya penalti, " kocha wa Uhispania Vicente del Bosque amesema. "Mchezo ulikuwa mgumu sana kwetu." ameongeza del Bosque.

Katika hali ya joto kali , kila upande uliweza kugonga mwamba wa goli katika dakika za nyongeza. Emmanuele Giaccherini alibamiza shuti lake katika mlingoti wa goli katika dakika ya 93 na Buffon alipangua mpira kutoka kwa Xavi Hernandez karibu na nguzo ya goli katika dakika ya 115.

"Ilikuwa ni juhudi za kutia moyo za wachezaji wa timu zote", Del Bosque amesema. "Ulikuwa ni mchezo safi na wachezaji wameonyesha juhudi za kimchezo ambapo mchezo huo ulichezwa katika mazingira magumu sana ya hali ya hewa."

Fainali itafanyika siku ya Jumapili katika uwanja wa Maracana mjini Rio de Janeiro. Italia itakumbana na Uruguay katika kutafuta mshindi wa tatu mjini Salvador pia siku ya Jumapili.

Spain head coach Vicente Del Bosque looks on prior to the World Cup quarterfinal soccer match between Paraguay and Spain at Ellis Park Stadium in Johannesburg, South Africa, Saturday, July 3, 2010. (AP Photo/Ivan Sekretarev)
Kocha wa Uhispania Vicent del BosquePicha: AP

"Hivi sasa tunapaswa kutafakari kile kinachotakiwa kufanywa katika muda wa siku hizi tatu za kurejesha nguvu," Del Bosque amesema . "Tutasimama kiume dhidi ya Brazil katika uwanja wa Maracana. Wachezaji wanapaswa kujisikia kama watoto wadogo wakicheza Maracana. Wameshinda mara nyingi , lakini wanataka kushinda katika uwanja wa Maracana."

Italia walitaka kulipa kisasi

Katika mchezo ambao ni marudio ya fainali ya kombe la mataifa ya Ulaya mwaka jana , ambapo Uhispania ilishinda kwa mabao 4-0, Italia ilionesha mchezo wa kutisha mapema kabisa katika mchezo huo hata bila ya mshambuliaji wao hatari Mario Balotelli, wakivizia kushambulia kwa kushtukiza, wakati Uhuspania iliamua kucheza mchezo wao wa kawaida wa pasi fupi fupi na kuumiliki mpira.

"Tumecheza mchezo mzuri. Tulitengeneza nafasi na kupoteza lakini kila mara tulikuwa tumo katika mchezo," Kocha wa Italia Cesare Prandelli amesema. "bado wako mbali na sisi lakini tunakuja juu na sisi. Ameongeza Prandelli.

"Katika mazingira kama haya , kati ya kuwakosa baadhi ya wachezaji na uchovu, ni vigumu kutumia nguvu zote, lakini vijana walifanya kazi nzuri na wamenifurahisha," Prandelli ameongeza.

Timu zilibadilishana muda wa kushambuliana katika kipindi cha pili lakini ilikuwa wakati wa dakika za nyongeza ndipo kila timu ikaweza kupata nafasi nzuri katika mchezo huo.

Mwandishi : Sekione Kitojo / ape