Conte awaonya wachezaji wake kutobweteka
1 Mei 2017Kocha wa viongozi wa ligi hiyo Antonio Conte amewaonya wachezaji wake kutobweteka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Everton na kufikiri kwamba ubingwa ni wao tu. Kikosi cha Conte kimejiimarisha katika nafasi yake juu kileleni mwa msimamo wa ligi, Jumapili, lakini timu iliyoko katika nafasi ya pili Tottenham inawafuatia nyuma kwa kasi ya ajabu.
Lakini wakati vijana hao wa Conte wakirejea nyumbani na ushindi huo , Tottenham walikuwa wanapata ushindi wao muhimu dhidi ya Arsenal na kujiweka katika nafasi ya kuitikisa Chelsea katika nafasi ya kwanza.
Hata hivyo kocha wa Arsenal, Aserne Wenger amesema hatasalim amri kuingia katika eneo la timu nne bora za juu katika Premier League msimu huu licha ya kipigo hicho cha mabao 2-0 dhidi ya Tottenham Hotspurs , hali inayoashiria kwamba Arsenal mara hii itamaliza chini ya mahasimu wao hao kwa mara ya kwanza katika miaka 21 kocha huyo akiwa katika klabu hiyo.
Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / dpae
Mhariri: Iddi Ssessanga