1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COPENHAGEN: Ndege ya abiria yawaka moto baada ya kutua kwa ghafla

10 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRC

Ndege moja ya abiria ya shirika la ndege la Scandinavia ilishika moto baada ya kutua kwa ghafla katika uwanja wa ndege wa Aalborg nchini Denmark.

Rubani wa ndege hiyo aliamua kutua ghafla baada ya kuyamwaga mafuta yote na kuripoti juu ya matatizo ya gia zinazotumiwa wakati ndege inapotua.

Muda mfupi baada ya kutua, ndege hiyo iliegemea upande mmoja na bawa la kulia na injini yake ikagonga barabara kabla kusimama. Rafadha moja ilivunjika na kuingia katika chumba cha ndege hiyo.

Polisi wanasema abiria wote 73 na wafanyakazi wanne wa ndege hiyo iliyokuwa njiani kutoka uwanja wa ndege wa mjini Copenhagen kwenda Aalborg, waliokolewa kabla ya injini ya bawa la kulia la ndege hiyo kuwaka moto. Moto huo ulizimwa haraka na wazima moto wa uwanja wa ndege wa Aalborg.

Abiria 11 walipekwa hospitalini kutibiwa kufuatia majeraha madogo waliyoyapata.