1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COPENHAGEN : Polisi yavunja maandamano

4 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMc

Kundi dogo la waandamanaji limewavurumishia mawe polisi na kutia moto madebe ya taka mjini Copenhagen hapo jana usiku na kuzusha hofu kwamba mji mkuu huo wa Danmark yumkini ukashuhudia usiku wa tatu wa ghasia.

Hali hiyo inakuja siku moja baada ya polisi kutumia mabomu ya kutowa machozi kuvunja maandamanao ya ghasia ya takriban watu 1,000 ambao walikuwa wanaadamana kupinga kuondolewa kwa wavamizi wa nyumba kutoka jengo la kituo cha vijana.

Waandamanaji walirusha mawe na mabomu ya petroli na kuyatia moto magari kadhaa.

Wajerumani kadhaa inasemekana kuwa ni miongoni mwa takriban watu 200 waliotiwa mbaroni.