1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Covid-19: Nchi za Ulaya zaondoa zafungua mipaka

Saleh Mwanamilongo
15 Juni 2020

Ujerumani na nchi za umoja wa Ulaya zinafungua mipaka na kuondoa tahadhari kwa ajili ya usafiri wa raia wa nchi 27 za umoja huo. Hata hivyo umoja huo utaendelea kufunga mipaka yake kwa watalii kutoka mengine duniani.

https://p.dw.com/p/3dm98
Polen EU-Grenzen sind wieder offen
Picha: picture-alliance/PAP/L. Muszynski

Ujerumani na nchi za umoja wa Ulaya zinafungua mipaka na kuondoa tahadhari kwa ajili ya usafiri wa raia wa nchi 27 za umoja huo. Hatua hiyo inaenda sambamba na pendekezo la kamisheni ya Umoja wa Ulaya linalozihimiza nchi wanachama kufungua mipaka kuanzia wiki hii. Hata hivyo umoja huo utaendelea kufunga mipaka yake kwa watalii kutoka Asia, Marekani na maeneo mengine duniani. 

Ujerumani na Ufaransa ziliondoa usiku wa kuamkia leo vizuizi vyao katika mipaka yao kama ilivyofanya Italia wiki mbili zilizopita.Hata hivyo raia wa Ujerumani bado wanashauriwa kuepukana na safari ambazo si za lazima nje ya nchi ambazo tahadhari hazijaondolewa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kuwa nchi yake inaondoa vizuizi vya kiuchumi vilivyowekwa, ikiwemo mikahawa yote kufunguliwa, ili kuharakisha juhudi za kufufua uchumi wa taifa hilo baada ya janga la corona. Kwenye hotuba yake kwa njia ya televisheni usiku wa kuamkia leo, Macron amesema nchi yake imerekodi ushindi wa kwanza dhidi ya COVID-19, na kwamba mikahawa katika mji wa Paris na viunga vyake itafunguliwa ili watu wale wakiwa ndani kuanzia leo Jumatatu, tofauti na hapo awali ambapo wateja waliruhusiwa kuketi tu nje ya mikahawa.

Frankreich Präsident Emmanuel Macron TV Ansprache
Picha: picture-alliance/abaca/L. Raphael

''Katika kupambana na janga la Corona, raia wetu,wakuu wa viwanda,wafanya kazi wa serikali, madaktari wauguzi walionyesha umakini,ushupavu na uzalendo na mshikamano ambao umetuwezesha kudhibiti wimbi hili ni lazima kuwapongeza katika ufanisi huo'', alisema Macron.

 

 Hofu ya wimbi jipya la maambukizi

Rais Macron pia ametangaza kuwa shule za msingi na sekondari zitafunguliwa kwa wanafunzi wote.Hata hivyo barani ulaya bado kuna tahadhari kuhusuiana na hatua hiyo ya kufunguliwa kwa mipaka,baada ya jumla ya vifo 182,000 kuripotiwa na maambukizi ya zaidi ya  watu milioni mbili miongoni mwa milioni 7.9  kote duniani,kwa mujibu wa taarifa za hospitali ya Chuo  Kikuu cha Jons Hopkins, Marekani.

Waziri mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez amesema kwamba nchi yake imeakhirisha hatua ya kufungua mipaka yake hadi Juni 21,akisema bado tishio lipo kutokana na uwepo wa virusi vya Corona. Huku Ugiriki ikitarajia kuwapokea watalii kutoka nchi za umoja wa Ulaya, Norway na Danemark zitaendelea kufunga mipaka yao na Sweden ambayo ni nchi ambayo haikuweka sheria za kutotoka nje wakati wote wa kipindi hiki cha janga la Corona.

Wakati ambapo Ulaya imefungua mipaka yake,kuna hofu ya kuzuka wimbi jipya la janga la Corona kufuatia China kuripoti visa vipya mwishoni mwa wiki iliyopita.