1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DÜSSELDORF: Kanada yataka vifaru vya Kijerumani nchini Afghanistan

24 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOv

Vifaru vya kisasa vya jeshi la Ujerumani,huenda vikapelekwa kusini mwa Afghanistan hivi karibuni. Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Kijerumani “Rheinische Post“ serikali ya Ujerumani huenda ikakubali ombi la serikali ya Kanada kupeleka vifaru chapa ya “Chui“ vilivyo na kinga imara dhidi ya mabomu yaliotegwa ardhini.Kanada,imeomba vifaru hivyo kuwalinda wanajeshi wake walio nchini Afghanistan,chini ya uongozi wa NATO kama sehemu ya vikosi vya kimataifa vinavyolinda usalama nchini humo ISAF.