1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dakar. Rais Wade athibitishwa mshindi.

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCK0

Baraza la katiba nchini Senegal limemtangaza rasmi rais Abdoulaye Wade kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika wiki mbili zilizopita.

Baraza hilo ambalo ndio chombo cha juu kabisa nchini humo kinachotoa maamuzi juu ya masuala ya uchaguzi limesema kuwa Wade ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 55.9 ya kura zilizopigwa.

Baraza hilo limetupilia mbali malalamiko ya vyama vya upinzani dhidi ya matokeo ya uchaguzi huo.