1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR. Wapiga kura wanamchagua rais nchini Senegal

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOi

Rais Abdoulaye Wade wa Senegal hii leo anagombea uchaguzi wa rais akitazamia kubakia madarakani kwa awamu ya pili.Wagombea uchaguzi wengine 14 pia wanapigania wadhifa huo.Rais Wade alishindwa mara nne katika chaguzi za rais na alibakia upande wa upinzani kwa kipindi cha miaka 26 kabla ya kufanikiwa safari ya tano katika uchaguzi wa mwaka 2000.Siku ya Ijumaa,katika mkutano wake wa mwisho wa kampeni,aliwaambia wafuasi wake ana hakika kushinda kwa urahisi.Kiasi ya watu milioni tano katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi wana haki ya kupiga kura.