1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Damascus. Kipindi cha rais kurefushwa.

28 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxY

Wapigakura nchini Syria wamekwenda kupiga kura katika kura ya maoni juu ya kurefushwa kipindi cha utawala cha rais Bashar al-Assad kwa miaka mingine saba.

Kura hiyo inaonekana kwa kiasi kikubwa kuwa ni hatua ya kawaida , wakati Assad anagombea bila kupingwa.

Bunge la Syria kwa kauli moja limempitisha Assad kugombea kwa kipindi cha pili katika kura iliyofanyika mwezi huu.

Bunge pia linatarajiwa kutangaza matokeo ya kura hiyo ya maoni leo Jumatatu.