1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Syria isaidie kuleta utulivu katika Mashariki ya Kati

4 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCma

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier alipokutana na waziri mwenzake Walid al-Muallem mjini Damascus,alitoa mwito kwa Syria kutumia ushawishi wake kwa chama cha Hezbollah, kumaliza maandamano yanayofanywa mji mkuu wa Lebanon,Beirut.Steinmeier alikutana pia na rais Bashar al-Assad wa Syria mjini Damascus, akipendelea kuiona Syria ikichangia kupata suluhisho la amani katika Mashariki ya Kati.Kwa mujibu wa Al-Muallem,suala lililo muhimu kwa Syria ni Israel kuondosha vikosi vyake kutoka Milima ya Golan.Hadi hivi sas, majadiliano kuhusu mada hiyo hayakufanikiwa.Syria ni kituo cha mwisho cha ziara ya siku nne ya waziri Steinmeier katika Mashariki ya Kati.