1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS : Syria yafanya uchaguzi tata wa bunge

22 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC81

Syria inafanya uchaguzi wa bunge wa siku mbili ambao vyama vya upinzani vilivyopigwa marufuku kushiriki vimesema kuwa hauna maana.

Kati ya viti 250 viti 167 vimetengwa kwa ajili muungano unaotawala unaongozwa na chama cha Baath cha Rais Bashar al Assad.Viti vyengine 83 vimetengwa kwa wagombea huru wengi wao wakiwa wafanya biashara.

Serikali ya Assad imeutangaza uchaguzi huo kuwa ni kioo cha demokrasia.