1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Syria yapendekeza kuisaidia serikali ya Irak

20 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCr9

Waziri wa mambo ya kigeni wa Syria, Walid al-Moualem, ametangaza utayarifu wa nchi yake kusisaidia serikali ya Irak. Ameyatamka hayo katika ziara yake mjini Baghdad.

Akiulizwa ikiwa ziara yake hiyo imefuatia mwito uliotolewa na waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair, Syria kuisaidia Irak, al-Moaulem amesema hakuenda nchini Irak kuyafurahisha mataifa ya kigeni yenye nguvu. Ameongeza kusema majeshi ya Marekani yangepaswa kuondoka kutoka Irak na kwamba hatua hiyo itapunguza mashambulizi ya waasi wa kiiraki.

Hiyo ilikuwa ndio ziara rasmi ya kwanza wa afisa wa serikali ya Syria nchini Irak tokea nchi hizo zisimamishe uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1982.