1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Wanajeshi takriban 15 wauwawa

26 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBex

Wanajeshi takriban 15 wameuwawa na wengine 50 kujeruhiwa kufuatia mlipuko uliotokea kwenye kambi kubwa ya jeshi karibu na mji wa Allepo kaskazini mwa Syria. Wanajeshi wengine 50 wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo na wamelazwa kwenye hospitali ya Kindi mjini Allepo.

Walioshuhudia mlipuko huo wamesema mlipuko huo ulitokea kwenye kambi ya kikosi maalumu na shule ya jeshi katika eneo la Muslemiah kaskazini mwa mji wa Allepo.

Maafisa wa Syria wamesema mlipuko huo si hujuma ya kigaidi, bali umetokea kufuatia joto kali huku kiwango cha joto kikiripotiwa kufika nyuzi karibu 50 kwenye kipimo cha Celcius. Joto hilo limesababisha ghala la silaha kulipuka.