1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Damu inazidi kumwagika nchini Irak

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2j

Baghdad:

Wanajeshi watano wa Marekani wameuliwa na watatu hawajulikani waliko kufuatia shambulio lililotokea leo kusini mwa Baghdad.Kwa mujibu wa uongozi wa kijeshi wa Marekani,mashambulio hayo yametokea kilomita 20 toka mji wa Mahmudiya-inakokutikana ngome ya waasi wanaoshirikiana na mtandao wa kigaidi wa al Qaida.Uongozi wa kijeshi wa Marekani umeongeza kusema wanajeshi sabaa wa kimarekani na mkalimani wao wa kiiraq walikua wakipiga doria katika eneo hilo.Juhudi za kuwasaka wanajeshi watatu waliopotea zinaendelea-taarifa ya uongozi wa kijeshi wa Marekani imesema.