1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM:marekani kuipa Tanzania dola 698 kuimarisha miundo mbinu

20 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOM

Marekani inaipa nchi ya Tanzania dola milioni 698 kuimarisha miundo mbinu na huduma za msingi nchini humo.Kampuni ya Millenium Change ya serikali ya Marekani MCC iliidhinisha hatua hiyo baada ya serikali ya Tanzania kuandaa mpango maalum wa kupunguza umasikini.

Msaada huo unalenga kukarabati barabara vilevile kuimarisha sekta ya nishati matatizo yanayorudisha nyuma maendeleo na kuweka vikwazo kwa wawekezaji.

Kampuni hiyo iliundwa mwaka 2002 na Rais George Bush ikiwa na lengo la kusaidia mataifa masikini yaliyo na nia ya kufanya mabadiliko.

Nchi za Madagascar,Cape Verde,Benin,Ghana,Mali,Msumbiji ,Lesotho na Morocco zimenufaika na mpango huo.