1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAVOS : Amani Mshariki ya Kati yawekewa nadhari

26 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXn

Juhudi za kufufuwa mchakato wa amani uliokwama Mashariki ya Kati zimewekewa nadhari katika siku ya pili ya Kongamo la Kiuchumi Duniani linalofanyika kwenye mji wa kitalii wa Davos nchini Swirtzerland .

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amekutana na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina pembezoni mwa mkutano huo.Hakuna maelezo yaliotolewa juu ya mkutano huo lakini Abbas amewambia waandishi wa habari kwamba anatarajia mambo mengi kutoka Ujerumani ambayo hivi sasa inashikilia Urais wa Kundi la Mataifa Manane yenye Maendelo makubwa ya viwanda duniani pamoja na Umoja wa Ulaya.