1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vurugu zaendelea Jamhuri ya Afrika ya Kati

2 Mei 2017

Makundi yenye silaha katika Jamhuri ya Afrika ya kati yamewaua raia wasiopungua 45 katika mapigano ya kisasi katika muda wa miezi mitatu iliyopita wasimamizi wa haki za binadamu walisema katika ripoti ya siku ya Jumanne.

https://p.dw.com/p/2cDfc
Menschen fliehen aus Zentral-Afrika
Watoto wakimbia vurugu huko Jamhuri ya Afrika ya KatiPicha: Reuters

Vurugu hizo zilisabishwa na mashambulizi ya vikundi vyenye silaha, zilisambaa  kati ya mkoa wa Ouaka, ambayo ni mpaka baina ya waislamu wa kaskazini na wakristo wa kusini nchini humo.

"Mvutano wa madaraka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati umewafanya wananchi wa kawaida kutoka pande zote kuathirika na mashambulio yanaoyofanyika," alisema Lewis Mudge, mtafiti wa mambo ya Afrika katika taasisi ya usimamizi wa haki za binadamu huko Marekani.

Jamhuri ya Afrika ya Kati imekuwa ikikabiliwa na vurugu la kisiasa tangu 2013 wakati kundi la waasi wa Seleka lililokuwa na wapiganaji wengi Waislamu lilipomng'oa madarakani rais Francois Bozize. Kundi hilo liliendelea kuuwa na kufanya  mashambulio, jambo ambalo liliwafanya wakristo nchini humo kuanzisha makundi na kijeshi ya kujilinda.

Hata baada ya uchaguzi wa kidemokrasia na kuapishewa kwa rais Faustin-Archange Touadera

March 2016 kundi la Seleka na makundi mengine yanaendelea kufanya vurugu nchini humo.

Mtu mmoja aliyeshuhudia shambulio la hivi karibuni, anayejulikana kwa Clemnet tu, alisema

wapiganaji wa kundi la Fulani Union for Peace Afrika ya kati, yaani Umoja wa Fulani kwa ajili ya amani, waliwapiga risasi watoto wanne na kuwauwa akiwemo mtoto wa miezi saba katika shambulio la mwezi wa Machi.

Wasimamizi wa haki za binadamu waliwafanya mahujiano na wakaazi kadhaa wa mji wa Barbaric mwezi wa April. Wazimamizi hao walisema kuwa kiwango cha watu walioathirika imepanda kidogo kwa sababu bado kuna wale watu waliopotea.

Umoja wa Mataifa ambao una walinda usalama 13000 katika nchi hiyo, ambayo ni koloni la zamani la Ufaransa. Wajumbe hao wamejaribu kufanya mashambulizi ya anga ili kuondoa makundi yanayofanya mashabulizi  huko Ouaka na kuendelea kuingia Barbaric.

Zentralafrikanische Republik Bangui Minusca UN-Truppen
Walinda usalama wa Umoja wa MataifaPicha: picture-alliance/AA/

Lakini bado vurugu zinaendelea nchi humo. Kundi la kutoka tiba za msaada la MS lilisema kuwa mwezi uliopita ulikuwa ni mwezi mbaya wa mashambulizi uliokuwa haujapata kutokea kwa muda mrefu. Kundi hilo pia liliripoti kuwepo kwa mauaji ya kikatili ya kukatakata na ya kunyonga.

Mwandishi: Najma Said/RTRE

Mhariri:Iddi Ssessanga