1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Del Bosque kujiuzulu baada ya Euro 2016

17 Oktoba 2014

Kocha wa timu ya taifa ya Uhispania - La Roja, Vicente del Bosque amethibitisha kuwa anapanga kujiuzulu baada ya kuiongoza timu hiyo katika dimba la mataifa ya bara la Ulaya - Euro 2016

https://p.dw.com/p/1DXw2
Bildergalerie WM 2014 Nationaltrainer
Picha: Reuters

Del Bosque ameliambia gazeti moja la Uhispania kuwa maishani, hauwezi kuwa na uhakika kuhusu kitu chochote lakini nia yake ni kuendelea kuwa kocha wa taifa hadi baada ya dimba la mataifa ya Ulaya litakaloandaliwa Ufaransa mwaka wa 2016.

Kocha huyo yuko katika mchakato wa kukijenga kikosi kipya cha Uhispania baada ya fedheha iliyotokea katika dimba la Kombe la Dunia nchini Brazil.

Mabingwa hao watetezi walishindwa kufuzu kutoka hatua ya makundi, hali iliyowalazimu magwiji Xabi Alonso, Xavi na David Villa wote kutangaza kutundika njumu zao katika soka la kimataifa.

Wameanza safari ya kufuzu katika Euro 2016 wakiwa na timu mpya ya chipukizi ambayo imepata ushindi mara mbili na kushindwa mara moja kufikia sasa katika Kundi C.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri:Yusuf Saumu