1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Deni kubwa kwa Ujerumani katika bajeti yake.

Sekione Kitojo24 Juni 2009

Baraza la mawaziri la serikali ya Ujerumani limefikia makubaliano juu ya bajeti ya nchi hiyo kwa mwaka 2010.

https://p.dw.com/p/IaWv
Waziri wa fedha wa Ujerumani Peer Steinbrueck akielezea kuhusu bajeti ya taifa.Picha: AP

Baraza la mawaziri la serikali ya Ujerumani jana Jumatano limefikia makubaliano kuhusiana na bajeti ya mwaka 2010. Katika kutayarisha tarakimu hizo waziri wa fedha Peer Steinbrück anapaswa kutilia maanani pia na kupambana na matokeo ya mporomoko wa kiuchumi. Mpango wake unaonekana kuielekeza Ujerumani katika deni kubwa kabisa.


Mtu anaweza kuiangalia hali hii yote kwa njia ya mzaha. Na tena kuna uzuri na ubaya wake. Kwa upande wa uzuri, ni kwamba serikali ya Ujerumani bado ina mafanikio , katika mpango wake wa bajeti kwa miaka ijayo , kwa upande wa mapato na matumizi kuweza kuwiana.

Na kwa upande wa habari mbaya, ni kwamba ni lazima kuchukua deni jingine la Euro bilioni 100. bajeti ya mwaka 2010 kwa sasa ina jumla ya kiasi cha Euro bilioni 327,7.

Pendekezo la bajeti ya mwaka 2010 inaanza kwa kuwa na deni kubwa kabisa lililopo linalokatisha tamaa. Karibu robo ya matumizi yote katika deni hili yanapaswa kubebwa na wananchi. Pamoja na kiasi cha Euro bilioni 86 waziri wa fedha Peer Steinbrück alizokadiria katika mapato jumla, ziada inakuja kiasi cha Euro bilioni kumu ikiwa ni deni jipya kwa ajili ya bajeti ya ziada. Kama hiyo haitoshi, katika mpango wa kipindi cha kati cha mpango wa fedha hadi mwaka 2013 kutakuwa na makadirio ya jumla ya Euro bilioni 310 katika deni la Ujerumani. Ujerumani kwa hiyo itakuwa imepitiliza kwa kiasi kikubwa katika urari wa bajeti katika kiwango dhidi ya mkataba wa kuimarisha sarafu ya Euro.

Kuna njia ya ubunifu, hali isiyokuwa ya kawaida inahitaji hatua zisizokuwa za kawaida. Katika kutekeleza hilo, hali ya kifedha ya majimbo inaonekana kuwa ya kawaida. Uchumi ulitumbukia katika mporomoko mkubwa baada ya mzozo wa kifedha wa mabenki. Hali ya ukuaji wa uchumi wa Ujerumani kwa mfano imepungua katika mwaka huu kwa kiasi cha asilimia sita. Hii haielekezi tu katika kupoteza mapato ya kodi kwa kiasi cha bilioni kadha, badala yake kuwa mzigo kwa bajeti ya taifa. Kwa upande wa mabenki ni lazima mpango wa uokozi ufungamanishwe na upande wa pili wa uchumi ambapo kuna mauzo ya dhamana za serikali zinazoweza kujenga daraja na kulegeza nguvu za mzozo huu. Kukiwa na mipango miwili ya kichocheo cha uchumi hali ya mahitaji ya mauzo ya nje iliyoharibika pia imerejea nyuma.

Bima ya kutokuwa na kazi inasisitiza kugharamia malipo mishahara yaliyoongezeka maradufu kwa wananchi kwa kiasi cha mabilioni ya Euro. Pia kwa upande wa ongezeko la malipo ya mafao ya kijamii, ni lazima kuamuriwa kufanya bora zaidi na kukubaliwa mapato ya kodi ya mashirika ya bima ya afya katika mwaka ujao yasitozwe kodi.

Kwa hiyo waziri wa fedha katika mwaka ujao kutokana na hali ilivyo hivi sasa ya utaratibu wa bajeti na kwa mwaka 2011 kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 40, anapaswa kuwasilisha bajeti ambayo mapato na matumizi yataweza kuwiana , ikiwa bila ya deni jipya.

Mwandishi Zawadzky, Karl/ZR

Aliyetafsiri Sekione Kitojo.

►◄