1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Deutsche Bahn latoa pendekezo jipya la mshahara.

21 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQ2Q

Frankfurt. Shirika la reli nchini Ujerumani Deutsche Bahn limeripotiwa kuwa limetoa pendekezo jipya la mshahara kwa madereva wa treni wanaogoma, wakati pande zote zikirejea katika meza ya majadiliano kujaribu kumaliza miezi kadha ya mzozo. Hakuna maelezo yaliyotolewa zaidi kutoka katika mazungumzo hayo baina ya kiongozi wa Deutsche Bahn Hartmut Mehdorn na kiongozi wa umoja wa madereva wa treni Manfred Schell. Migomo kadha ambayo imechukua muda wa saa 62 imesababisha mtafaruku mkubwa na kuligharimu taifa kiasi cha Euro milioni 75, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na shirika moja linalochunguza masuala ya kiuchumi. Chama cha waendesha treni GDL, kimekuwa kikidai ongezeko la mshahara la asilimia 31.