Deutsche Welle Facebook | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 17.09.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Deutsche Welle Facebook

Deutsche Welle inatoa nafasi ya kubadilishana mawazo na kujadiliana kupitia mitandao yake ya kijamii ya DW-WORLD.DE, Facebook, Twitter na majukwaa mengineyo.

Maingiliano ya kirafiki na ya kuheshimiana baina ya watu wanaotumia mitandao yetu hii ni muhimu sana kwetu.

Tafadhali wakati unaposhiriki katika mijadala, tumia lugha ya kiungwana na isiyokuwa na upendeleo, hata kama kunajitokeza kutofautiana kwa mawazo.

Tafadhali yakubali mawazo ya watu wengine wanaotumia mtandao huu; na jiepushe kumshambulia mtu binafsi. Watendee watumiaji wengine kama vile ambavyo wewe ungependa utendewe. Jiepushe kuandika kwa kutumia herufi kubwa zote, kwani hali hiyo inaweza ikatafsiriwa kuwa ni uchokozi. Pia jiepushe kurudiarudia kuweka vituo vya uandishi kama vile ?????? au !!!!!!!!

Unapotaka kunukuu watumiaji wengine au watu mashuhuri katika maoni yako, tafadhali elezea waziwazi chanzo cha habari.

Wakati unaponukuu maneno kutoka taarifa ambazo zina haki miliki, hakikisha una haki ya kisheria kufanya hivyo. Ikiwa huna hakika kama unayo au huna haki, ni bora ujiepushe kunukuu maandishi yenye haki miliki. Hii inahusiana na maandishi, picha za kawaida, picha za video, muziki na mengineyo.

Mambo yanayohusu ubaguzi wa rangi, maandishi au picha za ngono, za ubaguzi wa kijinsia, za kusababisha ushari na kuendeleza matumizi ya nguvu, yote hayo yataondolewa kwani yanaweza kuchochea au kuhamasisha vurugu na ghasia. Tafadhali jiepushe na aina yoyote ya uchochezi wa kisiasa. Vitendo hivyo haviruhusiwi kabisa.

Barua za mlolongo wa mapokezi (chain letters), barua pepe zilizotupwa (junk mails), barua pepe zisizotakiwa (spam) na maandishi ya matangazo au picha za biashara ni vitu visivyoruhusiwa. Maoni yoyote ya aina hiyo yataondolewa haraka. Deutsche Welle ina haki ya kuzuia na kuwaarifu watumiaji watakaokiuka maelekezo haya.

Hairuhusiwi kuchapisha taarifa binafsi, kama vile anuani za barua pepe au nambari za simu. Yaliyomo katika barua pepe binafsi au ujumbe kutoka mtu wa tatu, mbali na wale wawili walizotumiana, hayawezi kuchapishwa ikiwa hakujapatikana kibali.

Kumbuka kwamba maoni ni lazima yaambatane na maudhui ya kiuandishi tuliyoyatoa. Tafadhali jiepushe kutuma maoni ambayo kwa namna yoyote hayaendani na maudhui yetu.

Ili kuepuka kuchukua muda mrefu wakati wa ku-download tafadhali usidownload picha za video au sauti inayozidi dakika 10 au jalada la PDF lenye zaidi ya kurasa tano.

Ili kubadilishana kutoa maoni katika maudhui ya Deutsche Welle, si muhimu kujiandikisha. Maoni na barua pepe hazitochapishwa haraka katika tovuti ya DW-WORLD.DE, lakini yatachapishwa na msimamizi. Hii inaweza kuchukua wakati kidogo.

Deutsche Welle ina haki ya kufuta, kuondoa au kuyafunga maoni au mada yoyote. Hii pia inahusu maoni ambayo hayaendani na maudhui yetu ya kiuandishi.

Kwa kutumia au kushiriki katika jukwaa letu la mtandao wa kijamii wa kutoa maoni,kama vile Twitter, Facebook n.k., fahamu kuwa umekubaliana na mwongozo wa Deutsche Welle.

Furahia

Feedbackbutton: Kwa matatizo ya kiufundi au maswali, tafadhali bonyeza hapa kutuma barua pepe kwa idara ya uhariri.