1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA : Hati yatolewa kukamatwa waziri mkuu wa zamani

22 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC83

Mahkama ya Bangladesh imetowa hati ya kukamatwa kwa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Bibi. Hasina Wajed kwa madai ya mauaji.

Hasina kiongozi wa chama cha upinzani cha Awami League hivi sasa yuko London Uingereza na serikali ya Bangladesh inampiga marufuku kurudi tena nchini humo.Anatuhumiwa kwa kuhusika na mauaji ya watu wanne ambao walipigwa hadi kufa mjini Dhaka mwezi wa Oktoba mwaka jana.

Serikali ya Bangladesh inayoungwa mkono na jeshi inajaribu kuusafisha mfumo wa nchi hiyo uliotopea rushwa kwa kuwaweka uhamishoni Hasina na hasimu wake mkuu Khaleda Zia wa chama cha Nationalist Party.