1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA: Kimbunga SIDR kimeua watu 500 Bangladesh

16 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CImR

Si chini ya watu 500 wamepoteza maisha yao nchini Bangladesh baada ya kimbunga Sidr kuvuma kwa mwendo wa hadi kilomita 240 kwa saa.Serikali mjini Dhaka imesema,idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu bado watu wengi wanakosekana.

Kimbunga hicho kimesababisha mvua na mafuriko makubwa kusini-magharibi ya Bangladesh na kimeteketeza nyumba na vibanda.Mamia elfu ya watu wamelazimika kuondoka makwao.Umoja wa Ulaya umetoa Euro milioni moja na nusu kuwasaidia watu waliokumbwa na maafa yaliyosababishwa na kimbunga Sidr.