1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA: Polisi wazima maandamano

8 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcT

Polisi nchini Bangladesh wamekabiliana na waandamanaji katika mji mkuu Dhaka wanaotaka uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 22 mwezi huu uahirishwe.

Waandamanaji hao wanataka pia kufanyike mageuzi ya sheria za uchaguzi kabla uchaguzi huo kufanyika. Polisi wametumia marungu na gesi ya kutoa machozi kuwatanya waandamanaji.

Machafuko hayo yamezuka siku ya pili ya mgomo wa usafiri ulioitishwa na muungano wa upinzani unaongozwa na waziri mkuu, Sheikh Hasina. Muungano huo unasema rais Iajuddin Ahmed, anayeiongoza serikali ya mpito, anampendelea mpinzani mkuu wa waziri mkuu Hasina, Begum Khaleda, katika uchaguzi ujao.

Shughuli za kila siku zimetatizwa mjini Dhaka huku shule zikiwa zimefungwa na kukiwa hakuma magari katika barabara za mji huo.