1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA: Wanasiasa wakuu watiwa mbaroni Bangladesh.

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCV1

Vikosi vya usalama nchini Bangladesh vimetumia sheria ya hali ya hatari kuwakamata wanasiasa kadhaa wakuu na mawaziri wa zamani wa vyama mbalimbali vya kisiasa nchini humo.

Waliokamatwa ni washirika wa karibu wa waziri mkuu wa zamani, Bibi Khaleda Zia, na pia wanasiasa wakuu wa chama cha Awami kinachoongozwa na waziri mkuu wa zamani, Bibi Sheikh Hasina, ambaye ni mpinzani mkuu wa Zia.

Mzozo kati ya Bibi Khaleda Zia na Bibi Sheikh Hasina kuhusu marekebisho ya taratibu za uchaguzi umesababisha ghasia mabarabarani miezi ya hivi karibuni hadi ya kumfanya Rais Iajuddin Ahmed kutangaza hali ya hatari nchini humo tarehe kumi na moja mwezi uliopita.

Uchaguzi uliopangwa kufanywa mwishoni mwa mwezi uliopita uliahirishwa na serikali ya muda inayotakikana kuusimamia uchaguzi huo imeapa itapambana vikali na ufisadi kwenye midani ya kisiasa na pia serikalini.