1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA:Amri ya kutotoka nje yaondolewa

28 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVI

Serikali ya mpito ya Bangladesh inayoungwa mkono na jeshi la nchi hiyo imeondoa amri ya kutotoka nje iliyoiweka katika mji wa Dhaka na maeneo mengine matano kutokana na maandamano ya wanafunzi yaliyokuwa yametapakaa.

Wizara ya mambo ya ndani ilitoa taarifa ya kuondoa amari hiyo hapo jana jioni ikisema utulivu na amani umerudi.

Serikali ya mpito ilitangaza hali ya kutotoka nje jumatano iliyopita baada ya kuzuka na kuenea kote nchini maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dhaka dhidi ya kuwepo wanajeshi katika mechi ya kabumbumbu katika chuo hicho.Maandamano hayo yalisababisha kuuwawa kwa mtu mmoja na kujeruhiwa wengine kiasi cha 300.Serikali pia ilifunga mara moja hadi muda usiojulikana vyuo vyote katika mji wa Dhaka na miji mingine mikubwa nchini humo.

Serikali ya mpito imekuwa ikiwashutumu wanafunzi na baadhi ya walimu wanaungwa mkono na vyama vya upinzani kwa kujaribu kuleta hali ya msukosuko nchini.